Idara ya Kilimo ilianza mwaka 2013 baada ya kutenganisha idara mama ya kilimo na mifugo.
MAJUKUMU YA IDARA YA KILIMO.
-Kutoa elimu ya kilimo bora kwa wakulima ili kuwezesha wakulima kuongeza tija katika uzalishaji .
-Kusimamia miradi ya kilimo
-kutoa elimu ya hifadhi bora ya mazao ili kuzuia upotevu na hivyo kupunguza hasara inayotokana na upotevu na uharibifu wa mazao.
-Kutathimini visumbufu vya mazao na kutoa taarifa kwa taasisi zinazoshughulika na udhibiti wa visumbufu vya mazao.
-Kuratibu na kusaidia upatikanaji wa pembejeo (mbegu bora, mbolea na viuatilifu) kwa wakulima .
-Kushirikiana na jamii katika kuandaa miradi ya kilimo ambayo inatokana na hitaji la wakulima wenyewe.
-Kukusanya taarifa za hali ya hewa na kuziwasilisha kwa wakulima kwa ajili ya kujiandaa na kalenda ya kilimo msimu unaofuata.
-Kutoa ushauri kwa wakulima juu ya kilimo cha mazao yanayostahimili ukame kwa vile wastani wa mvua katika wilaya hii ni kati ya 450mm hadi 950mm kwa mwaka , wastani ambao ni kidogo sana na haufai kwa kulima mazao yanayohitaji maji mengi na muda mrefu kukomaa.
-Kueneza teknolojia mpya ya kilimo kama vile mbegu bora, mbegu kinzani na magonjwa na wadudu,kutumia zana au nyenzo bora za kilimo.
-Kuandaa na kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kilimo kwa baraza la madiwani na kamati za kudumu za Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.
-Kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia mpya.
HUDUMA ZA KIJAMII.
-Kufanya tathimini ya hali ya chakula (usalama wa chakula)
-Kutoa elimu ya hifadhi na matumizi bora ya chakula kwa wakulima.
-Kutoa mafunzo kwa wakulima.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa