• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii

Maendeleo ya Jamii

  • UTANGULIZI:

Idara ya Maendeleo ya Jamii ni idara kiungo kati ya jamii, Serikari na wadau mbalimbali wa maendeleo. Idara ya Maendeleo ya Jamii ina vitengo (Section) kama ifuatavyo:-

  • Sekta cha vijana
  • Sekta ya kudhibiti UKIMWI
  • Dawati la jinsia  
  • Sekta ya Uratibu wa shughuli za NGOs.

Kama Idara mtambuka idara hushirikiana na idara nyingine katika Halmashauri ya Wilaya  pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali na Asasi za kiraia zilizopo katika maeneo ya Wilaya hii.

  • HALI YA WATUMISHI

Idara ina jumla ya watumishi 22 ambao wako makao Makuu na ngazi ya Kata kwa mchanganuo ufuatao:-

  • Ngazi ya wilaya watumishi 8
  • Ngazi ya kata watumishi 14
  • MAJUKUU YA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII JINSIA, WAZEE NA WATOTO

Shughuli zinazotekelezwa  na idara hii ni pamoja na :-

  • Kuhamasisha jamii kubuni, kupanga, kutekeleza, kusimamia na kutathimini mipango na miradi yao ya maendeleo.
  • Kuelimisha jamii kuondokana na mila zenye zilizopitwa na wakati na kuwa na mtazamo wa kupenda mabadiliko chanya.
  • Kuhamasisha jamii juu ya matumizi ya teknolojia rahisi na sahihi kwa kutumia rasilimali  zilizopo na zinazopatikana kwa urahisi.
  • Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutoa taarifa na matukio mbalimbali kama vifo, milipuko ya magonjwa, masoko, uzalishaji mali, vyakula, ajira na unyanyasaji wa kijinsia.
  • Kuratibu shughuli zote za maendeleo zinazosimamiwa na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) katika Wilaya.
  • Kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na matatizo mbali mbali yanayorudisha nyuma maendeleo katika jamii kwa kushirikiana na watumishi wa sekta zingine.
  • Kusimamia na kuratibu shughuli za maendeleo ya wanawake, vijana, watoto na wazee.
  • Kuhimiza, kujenga na kuimarisha ari ya kufanya shughuli za maendeleo kwa kujitolea katika maeneo yao.
  • Kueneza elimu ya uraia mwema kwa jamii
  • Kutoa elimu kwa jamii ili kuepukana na maambukizi  ya VVU/UKIMWI.
  • Kusimamia, kusambaza, kuelimisha jamii juu ya sera mbalimbali za maendeleo ya jamii kuanzia ngazi ya jamii.
  • HUDUMA ZA KIJAMII

Idara ya maendeleo ya Jamii inatoa huduma mbalimbali za kijamii kwa ajili ya kuhakikisha jamii inapata maendeleo inayoyahitaji:-

  • Kusajili vikundi vya vijana, wanawake na makundi ya mchanganyiko (wanawake na wanaume)
  • Kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa makundi mbalimbali ya wajasiriamali wadogo wadogo ili kuinua mitaji yao
  • Kutoa misaada kwa makundi maalumu (walemavu, watoto yatima, wajane, watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi)
  • Kusaidia wafungwa wa muda mfupi  kutoka gerezani na kupangiwa kazi za nje
  • Kutoa elimu ya kujitambua na afya ya uzazi kwa wanafunzi wa shule za sekondari
  • Kutoa msaada wa mitaji midogo midogo kwa makundi ya kijasiriamali ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI
  • MATARAJIO YA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
  • Idara inatarajia kuendelea kuwawezesha makundi ya vijana na wanawake miradi midogomidogo ya ujasiriamali.
  • Idara inatarajia jamii kuongeza uwezo wa kuibua na kuzitumia fursa zilizopo ndani ya maeneo yao ili kuleta maendeleo endelevu.
  • Idara inatarajia jamii itapata uelewa wa kuepukana na mila zilizopitwa na wakati ili kujenga jamii yenye ushirikiano.
  • Idara inatarajia ukatili wa kijinsia uendelea kupungua aidha wanawake wamejengewa ujasiri wa kujiamini katika mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na ushiriki katika maswala ya kijamii.
  • Idara inatarajia kuona jamii inajitambua na kuondokana na fikra tegemezi
  • Idara inatarajia jamii kuwa na uelewa wa sera na miongozo mbalimbali inayotelewa kwa ajili ya maendeleo yao.
  • Idara inatarajia jamii hasa vikundi vya wanawake na vijana vinavyopata mikopo kwa riba nafuu kuongeza kipato hivyo kupunguza au kuondoa dhana ya utegemezi.

Matangazo

  • Tangazo la kazi kada ya Afya December 12, 2018
  • Majina ya walioitwa kwenye usaili nafasi ya watendaji May 10, 2018
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • OPE yafanya Tathimini juu ya Mimba na Ndoa za Utotoni

    February 04, 2021
  • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango kukagua Miradi ya Maendeleo

    February 02, 2021
  • Milioni 34.4 kunufaisha Vikundi vya Ujasiriamali Kushapu

    January 18, 2021
  • Wanafunzi Waaswa Kusoma kwa Bidii Wakizingatia Uzalendo

    January 11, 2021
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa