Kamati za kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ziko tatu (3) ambazo ni;
i) Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala.
ii) Kamati ya Afya, Elimu na Maji.
iii) Kamati ya Mazingira, Uchumi na Ujenzi.
1. Majukumu ya kamati ya Fedha, Mipango na Utawala ni;
- Kuweka mikakati ya kuongeza mapato na kupendekeza njia za kuongeza mapato ya Halmashauri.
- Kuwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango wa maendeleo kwa Halmashauri.
- Kufuta madeni na kuomba vibali maalum kwa matumizi yanayoitaji idhini ya waziri mwenye dhamana ya Serikali za mitaa.
- Kusimamia utunzaji wa hesabu za fedha na uhakiki wa mali za Halmashauri.
2. Majukumu ya kamati ya Afya, Elimu na Maji. (Huduma za kijamii) ni;
- Kuandaa mipango ya ujenzi na upanuzi wa hospitali, vituo vya afya na zahanati.
- Kusimamia utekelezaji wa huduma za Afya ya msingi na kampeni za afya ya jamii
- Kuandaa mipango ya ujenzi na upanuzi wa shule za awali, msingi na sekondari.
- Kupendekeza miradi ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
- Kupanga na kusimamia miradi ya upatikanaji wa maji safi na salama vijijini na mijini.
3. Majukumu ya kamati ya Mazingira, Uchumi na Ujenzi ni;
- Kupanga na kupendekeza mipango ya kupanua biashara na kuongeza mapato ya Halmashauri.
- Kupendekeza na kusimamia miradi ya ujenzi wa barabara, majengo ya umma na miundombinu mingine.
- Kupendekeza mipango ya matumizi ya ardhi katika eneo la halmashauri.
- Kupendekeza mikakati ya kupunguza athari za uharibifu wa mazingira.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa