Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese amewaasa wanafunzi wa kike kuishi hosteli ili kuepuka vishawishi wanavyoweza kukutana navyo.
Kengese ametoa rai hiyo Machi 8, 2018 alipozungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Mangu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kiwilaya kijiji cha Ndoleleji.
Alisema kuwa Serikali inatumia fedha kujenga miundombinu hiyo ili kuwajengea wanafunzi mazingira mazuri ya kujisomea na kujiandaa vyema na mitihani yao.
“Tusome tuache mambo mengine yasiyo na maslahi kwetu hapa tunayo hosteli lakini hatuitumii huko nje tunapoenda kuishi si salama kwani vishawishi ni vingi mnaweza kupata mimba,” alisisitiza.
Katika maadhimisho hayo yaliyoshirikisha wadau Agape, Save the Children International, Redeso na World Vision wanafunzi hao walikabidhiwa zawadi mbalimbali zikiwemo kilo 100 za mchele, madaftari na mafuta ya kupikia.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa