Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba amewataka wataalamu kila mmoja atimze wajibu wake katika kuongeza nguvu katika ukusanyaji mapato ili kufikia malengo ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mhe. Taraba ametoa mwito huo Septemba 14, 2018 wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Alisema kuwa ili tuweze kupata mapato ya kutosha ni lazima kila mmoja atimize wajibu wake mahali pake kuanzia watendaji hadi madiwani na wananchi kwa ujumla.
“Sisi hatuna viwanda vikubwa wala masoko lakini tukisimamia vizuri katika vyanzo vya mapato yetu madogo madogo tutapata mapato ya kutosha na hatimaye miradi yetu ya maendeleo tutaijenga,” alisema Mhe Taraba.
Aidha, kwa upande mwingine alisema katika msimu huu mpya wa uzalishaji tunapaswa kujipanga na kurekebisha changamoto zilizokuwepo mwaka jana na kuzalisha zaidi.
Mkuu huyo wa wilaya alifafanua kuwa endapo watazalisha zaidi wataweza kumaliza changamoto hizo ndogondogo pamoja na kukusanya mapato kwa kiasi kikubwa.
Aliwataka viongozi kuhakikisha wakulima wanachangamkia matrekta ya mkopo kutoka serikalini ili kuweza kupata mavuno mengi zaidi na hivyo Serikali kupata mapato ya kutosha.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa