Maadhimisho ya siku ya Wanawake wilayani kishapu mkoani Shinyanga yamefanyika leo tarehe 06 March 2020 ambao mgeni rasmi Mheshimiwa Nyabaganga Taraba ambaye ni Mkuu wa Wilay ya Kishapu ameongoza maathimisho hayo yenye kauli mbiu “kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya sasa nay a baadaye” yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mwigumbi katika kata ya Mondo na kuhudhuriwa na wanawake kutoka sehemu mbalimbali wilayani Kishapu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa haki za Wanawake ikiwemo TGNP.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa wilaya ya Kishapu aliwakumbsha wanawake kuwa wao ni watu jasiri na sio waoga hivyo wanapaswa kusimama kwa ajili ya maendeleo ya familia zao na jamii kwa ujumla.
“Wanawake sio watu wa kawaida , bila wanawake haya maendeleo yasingekuwepo hivyo msiogope kujihusisha katika shughuli za maendeleo kwa kusubiri kuwezeshwa. Wanawake ni watu wenge upendo hivyo tupendane na kusaidiana katika harakati za mandeleo. Leo nawafundisha kanuni ya kutoa mambo yote mabaya na kuongeza mambo yote mazuri yatakayo tufikisha kwenye maendeleo. Wanawake tuna nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko kwenye jamii, hivyo tufanye kazi kwa bidii kwan iukiwa na kipato chako hakuna mwanaume atakaye kufanyia ukatili” alisema Taraba.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alikumbusha wazazi kuwajibika katika malezi ya watoto wao ikiwemo na kuwapeleka shuleni kusoma kusoma kwani ndio urithi wao kwa maisha yao ya baadaye.
“Ndugu zangu ili uweze kusonga mbele na kufikia malengo yako ni lazima upate msingi wa elimu ili mfumo wa maish ya baadeye uwe mzuri, hivyo wazazi tusomeshe watoto wetu. Nanyi watoto wa kike kataeni mimba ili muweze kutimiza ndoto zenu” aliongeza Taraba
Kwa upande wake Katibu wa Vituo vya Taarifa na Maafa wilayani Kishapu vinavyosimamiwa na TGNP, Peter Nestory aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kupinga ukatili wa aina zote ikiwemo uwakilishi sawa katika vyombo vya maamuzi na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
“iwakilishi katika vyombo vya maamuzi kama vile katika serikali za vijiji na mita, udiwani, ubunge na mabaraza mbalimbali yanasaidia kumuwezesha mwanamke kupaza sauti ili kufukia mpango wa usawa wa 50% kwa 50% baina ya wanawake na wanaume ” alisema Nestory.
“Ili kufukia malengo ya 50% kwa 50% ni lazima wanawake wajitokeze kwenda kugombea nyadhifa mbalimbali za uongozi kwani bado idadi ya viongozi wanawake ni ndogo. Mikakati inahitajika ili kufikia malengo ya usawa kwenye uonozi ifikapo 2030” aliongeza Nestory.
Naye Mwanaharakati wa Haki za wanawake,Fredina Saidi ambaye amekuwa mchango mkubwa katika harakati za ukombozi wa wanawake akipigania agenda za wanawake tangu mwaka 2003 aliwataka wanawake wanaogombea nafasi mbalimbali za uongozi kutokukata tama.
“kama una nia ya kuwa kiongozi simama imara, usitetereke wala kujali kauli zinazovunja moyo ikiwemo ile ya ‘mwanamke akiwa kiongozi atashindikana na kuwakalia wanaume’ kuwa jasiri na amini unaweza kuwa kiogngozi” alisema Saidi.
Katika maadhimisho hayo Halmashauri ya wilaya ya Kishapu kwa kusharikiana na wadau mbalimbali Wa haki za wanawake na watoto wakiwemo CRDB Bank walitoa misaada mbalimbali kwa watoto na wanawake wanaoishi katika mazingira magumu ikiwemo kutelekezwa na waume zao. Misaada hio ni kama vile chakula, madaftari, kalamu na pedi.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa