Kamati ya Fedha, utawala na Mipango (FUM) pamoja na Wataalamu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imefanya ziara ya siku mbili kuanzia tarehe 11 Mei 2020 hadi tarehe 12 Mei 2020 ili kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na fedha za serikali pamoja na wadau wa maendeleo.
Ziara hio ilioongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mheshimiwa Boniphace Butondo ambapo wajumbe waliweza kuangalia utekelezaji wa miradi pamoja na kuhoji matumizi ya rasilimali fedha zilizoelekezwa kwenye miradi.
Aidha wajumbe waliweza kubainisha shughuli wanazofanya watendaji wa serikali, mafanikio pamoja na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo kutimiza majukumu yao.
Miradi iliyotembelewa ilihusisha idara mbalimbali ambazo ni Afya, Elimu Msingi, Utawala na Kilimo. Katika idara ya Afya wajumbe walitembelea Zahanati ya Seseko na Kituo cha Afya Mwigumbi. Katika idara ya Elimu Msingi wajumbe walitembelea Ujenzi wa matundu 24 ya vyoo katika Shule ya Msingi Buchambi. Ujenzi wa Nyumba ya Walimu Shule ya Msingi Imala Bupina. Ukamilishaji wa nyumba ya Walimu (two-in-one) Shule ya Msingi Isoso. Idara ya Utawala wajumbe walitembelea Mradi wa Ukamilishaji wa Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Mwamalasa. Katika idara ya Kilimo wajumbe walitembelea Jengo la Resource Centre Mwamalasa.
Aidha, kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ina dhamana kubwa kusimamia fedha zinazotekelezwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo kama Afya, Elimu, Kilimo, Ujenzi pamoja na sekta nyingine, lengo ikiwa ni kuhakikisha kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya miradi zinafanya kazi iliyokusudiwa kikamilifu.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa