Wajumbe wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania(ALAT) kutoka Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga wametembelea miradi mbalimbaliya maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Geita mkoani Geita ikiwa ni ziara yamafunzo.
Katika ziara hiyo wajumbe hao kutoka Halmashauri zaWilaya ya Kishapu, Ushetu, Msalala, Shinyanga, Mji wa Kahama na Manispaa yaShinyanga walijifunza namna wenzao wanavyokusanya mapato kupitia miradimbalimbali ikiwemo ya mgodi wa dhahabu.
Akitoa maelezo kuhusu mafanikio ya miradi naukusanyaji mapato Mkurugenzi wa Mji huo, Mhandisi Modest Apolinary alisemaHalmashauri kwa upande wa ukusanyaji mapato imekuwa ikipanda mwaka hadi mwaka.
Mhandisi Apolinary alitolea mfano hali halisi hivisasa ambapo ni robo ya pili alisema imefikia zaidi ya asilimia 70 ya ukusanyajina kuwa wanatarajia kiwango kitapanda zaidi na kufikia asilimia 200.
Aidha alisema kutokana na mapato kuwa makubwa nawananchi kuamka kulipa ushuru mbalimbali Geita Mji imejenga soko kubwa na lakisasa lenye thamani ya sh. bilioni 2.
Soko hilo lililozinduliwa hivi karibuni na WaziriMkuu Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ziara mkoani humo limetembelea pia naujumbe wa ALAT Mkoa wa Shinyanga.
Kupitia soko hilo ambalo limejengwa kwa mapato yandani limeelezewa kuwa litatoa ajira kwa wananchi kutokana na shughulimbalimbali zitakazofanyika hapo pamoja na maduka makubwa.
Aidha, kwa mujibu wa Mkurugenzi Halmashauri hiyoinajenga shule mpya 10 za msingi na tano za sekondari katika mwaka huu wa fedhaambazo kukamilika kwake kutainua kiwango cha elimu.
“Kila mwaka tunakuwa na watoto wengi wanaohitajikuanza shule hivyo tumeona tupunguze changamoto ya upungufu wa madarasa iliwatoto wasome na tunafanya hivi wananchi waone kodi wanayotoa inafanya kazikweli,” alisema.
Kwa upande wake Mweka Hazina wa Mji, MunguabelaKakulima alitoa siri ya mafanikio katika ukusanyaji mapato kuwa ni ushirikishwajiwa idara zote.
Alisema kila wiki vikao vya Timu ya Wataalamu ajendayake kuu ni mapato na kila idara yenye chanzo inashiriki katika mazoezi yaukusanyaji mapato badala ya kuiachia Idara ya Fedha pekee.
“Hapa tuna ushirikiano mkubwa na ukikwama sote kwapamoja kama timu tunasaidia na pia tunafanya kazi kwa uwazi kwakushirikishana,” alidokeza Kakulima.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa