Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa kushirikiana na Shirika la Relief for Development Society (REDESO) imezindua Kamati ya Maafa Wilaya katika kikao kilichofanya wilayani humo.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya itakuwa na jukumu la kumshauri Mkuu wa Wilaya ya Kishapu kuhusu utekelezaji wa shughuli za usimamizi wa maafa zinazotekelezwa.
Aidha itasimamia utekelezaji wa mipango ya kukabiliana na maafa pamoja na kutafuta fedha na rasilimali nyingine zinazohitajika kwa ajili ya kupunguza athari za maafa.
Kwa kushirikiana na Taasisi ya kusimamia maafa ngazi ya Taifa na ngazi ya Mkoa, kuamrisha watu watu kuhama maeneo hatarishi au maeneo yenye mwelekeo wa kuathirika kutokana na maafa na kuwapeleka sehemu nyingine inayostahili.
Katika kikao cha uzinduzi wa kamati hiyo yenye wajumbe wakuu wa idara na vitengo pia itasimamia na kuratibu shughuli za kukabiliana na maafa katika Halmashauri walipitia muundo wake.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa