Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imekabidhi jengo jipya la maabara kwa Shule ya Sekondari Mangu iliyopo Kata ya Shagihilu baada ya ukarabatiwake kukamilika.
Maabara hiyo iliyokamilika gharama ya thamani yaSh. Milioni 10.1 linatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo wamchepuo wa sayansi kwa vitendo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya yaKishapu, Mang’era Mang’era akikabidhi jengo hilo alisema litachochea ufaulu wawanafunzi ambao awali walikosa mazoezi ya vitendo.
Alisema lengo la Halmashauri ni kuhakikisha elimuinakua na hivyo inaendelea kuboresha miundombinu ya shule zake ikiwemo ujenziwa maabara kwa ajili ya sayansi.
Mang’era Mang’era aliwataka walimu na wanafunzikuwa kitu kimoja na kuitendea haki maabara hiyo kwa kushirikiana ili wawe naufaulu mzuri katika mitihani inayohusisha mazoezi ya vitendo.
Alisema kuwa ufaulu kwa wanafunzi katika shulehiyo na zingine utafaleta sifa kwa wananchi wa kata hiyo pamoja na Halmashauriya Wilaya ya Kishapu kwa ujumla.
Mang’era ambaye pia ni Afisa Mipango aliwatakawanafunzi kuwa na nidhamu na kusoma kwa bidii ili kuweza kufikia malengo yao yabaadaye katika kitaaluma.
Aidha aliwashukuru wananchi kwa kushiriki katikashughuli za maendeleo ikiwemo kuchangia nguvu kazi katika kufanikisha ujenzi wajingo hilo la maabara.
Alisema juhudi za wananchi zimefanikisha ujenzi wamaabara hiyo ambao wamekuwa wakichangia nguvu kazi katika maendeleo yao kama ambavyo Serikali imekuwa ikisisitiza.
Shule za sekondari Mangu yenye wanafunzi wa kidatocha kwanza hadi cha nne inatarajiwa kupandishwa hadhi na hatimaye kuanzakuchukua wanafunzi wa kidato cha tano na sita,
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa