Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imepangiwa jumla ya walimu 44 watakaojaza nafasi katika shule za msingi na sekondari baada ya mchakato wa kutangaza ajira za watumishi wa kada hiyo.
Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo jumla ya walimu 4840 wamepangiwa katika shule mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kibali cha ajira cha kuajiri walimu 6840.
Mhe. Jafo alibainisha kuwa kibali kilichotoka Mei 30, 2018 kilitoa nafasi ya kuajiri walimu 4785 wa shule za msingi, 55 mahitaji maalumu na walimu 2000 wa sekondari wanaofundisha masomo ya sayansi kwenye shule za sekondari ambao mchakato wake bado unaendelea.Alifafanua kuwa walimu waliotangazwa ni wale waliotuma maombi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Desemba 2017 na walimu 2767 walipangiwa vituo vya kazi Januari 2018.
Aidha, Waziri huyo aliwatakaa walimu waliopata nafasi kuripoti katika vituo vyao vya kazi kuanzia Julai 23, 2018 hadi tarehe 7 Agosti 2018 wakiwa na vyeti halisi vya taalumu na cha kuzaliwa.
Alitoa maelekezo walimu wote wamepangiwa vituo vya kazi na si makao makuu ya Halmashauri na kuwa mwajiriwa yeyote atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu kisha akaondoka Serikali itamchukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.
Alisisitiza hakuna mwalimu atakayekubadiliwa kubadilishiwa kituo kwa sababu yoyote na watakaoshindwa kuripoti kwa muda uliopangwa nafasi zao zitachukuliwa na walimu wengine 5,220 wenye sifa waliokosa nafasi katika awamu hii.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa