Halmashauri imetenga jumla ya sh. milioni 107.68 kupitia mapato yake ya ndani zitakazotumika kuboresha miundombinu ya shule zake za sekondari.
Fedha hizo kwa ujumla wake zitatumika kujenga vyumba vinane vya madarasa, nyumba nne za walimu na matundu 18 ya vyoo kwa shule zake za sekondari.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Stephen Magoiga ambapo amesema pia inatarajia kupokea kiasi kingine kutokana na Mradi wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (SEDP II).
Alisema kuwa jumla ya sh. milioni 390 zinatarajiwa kutolewa na SEDP II kwa ajili ya ujenzi wa vyumba sita vya madarasa pamoja na nyumba sita za walimu.
Aidha, Magoiga aliongeza kuwa kupitia Ruzuku ya Maendeleo (LGDG) kiasi cha sh. milioni 48 zinatarajiwa kutolewa kwa ajili ya ujenzi nyumba nne za walimu wa sekondari.
Aidha, Halmashauri inaendelea kuhamasisha wadau wa maendeleo kama vile TCRS, EMEDO, OXFAM na jamii kwa ujumla katika kuchangia shughuli za maendeleo.
Kutokana na mikakati hiyo itaweza kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu hususan ya sekondari kwenye shule zake.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa