Kamati ya Fedha,Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ikiambatana na Wataalam wa Halmashauri imefanya ziara ya siku mbili kuanzia Februari 1, 2021 hadi Februari 2, 2021 katika tarafa za Negezi, Mondo na Kishapu ili kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Lengo la ziara ni kukagua miradi ambayo inatekelezwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya kujiridhisha na namna ambavyo miradi imetekelezwa ili kuona kama utekelezaji wa miradi unaenda sambamba na thamani ya Fedha ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri na mapendekezo pale wanapobaini mapungufu.
Ziara hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. William Jijimya ililenga kutembelea miradi ya maendeleo ikiwa ni ujenzi wa bweni l Wasichanana madarasa 4 Shule ya sekondari Ukenyenge, Ujenzi wa matundu 6 ya vyoo Kituo cha Afya Nhobola, Ukarabati mkubwa wa majengo ya shule, ujenzi wa vyumba vya madarasa 2 pamoja na ujenzi wa bweni shule ya sekondari Mwadui Ufundi, ukarabati mkubwa wa majengo ya shule ya sekondari Shinyanga, Ujenzi wa madarasa 4 shule ya sekondari Talaga, ujenzi wa madarasa 4 shuleya sekondari Masagala, ujenzi wa matundu 4 ya vyoo kituo cha Afya Songwa, ujenzi wa matundu 6 ya vyoo kituo cha Afya Kishapu na ukarabati wa vyumba 3 vya madarasa na matundu 6 ya vyoo shule ya sekondari Isoso.
Ziara ilikuwa ya mafakinikio ambapo jumla ya miradi 13 imetembelewa na kukaguliwa na kamati ya fedha Utawala na Mipango ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa halmashauri ili kutekeleza miradi hio kwa muda maalumu uliotengwa.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa