Kamati ya Afya wilayani Kishapu leo tarehe 27 mei 2020 imefanya kikao kujadili mwenendo wa Afya katika wilaya ya Kishapu. Mwenyekiti wa Kamati hio Sostenes Mbwilo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu aliwasisitiza wajumbe wa kamati kila mmoja kujua wajibu wake katika kamati hio na kuyasimamia ipasavyo ili kuinua hali ya lishe katika kata na wilaya kwa ujumla.
Hali ya Lishe katika wilaya ya Kishapu imeimarika kwa kiasi kikubwa ambapo watoto wachanga na wajawazito wamepatiwa huduma za afya kikamilifu pia akina mama wenye watoto wachanga wamepatiwa elimu ya Afya na namna ya kuboresha afya zao. Kadhalika, wahudumu wa afya ngazi ya jamii wamepata mafunzo kuhusu kugundua na kutibu utapiamlo pamoja na mbinu mbalimbali za kuboresha lishe na kupunguza ulemavu kwa watoto wachanga.
Kwa mujibu wa kikao hicho hali ya lishe kiwilaya inaonekana kuimarika ambapo miradi mbalimbali ya lishe kama vile mradi wa Viazi Lishe ambao uko chini ya Enrich umewafikia wananchi kwa asilimia kubwa. Emanuel Balibate ambaye ni Afisa Ufuatiliaji na Tathimini Enrich amesema Viazi Lishe vina Vitamin A na virutubisho vingine ambavyo ni muhimu kwa afya ya ngozi na kinga dhidi ya maradhi mbalimbali hivyo kamati ihakikishe inafanya mradi huu kuwa endelevu na mdau kutatua changmoto za mradi kabla hajakabidhi na kuwajengea uwezo wanaoachiwa mradi ili kuufanyia kazi kikamilifu.
Naye Afisa Uchechemuzi na Mawasiliano Jukwaa la Lishe nchini (PANITA), Faraja Kassim ameisisitiza kamati kuhakikisha kuna fesha za kutosha kwa ajili ya kuendesha shughuli za lishe kuanzia ngazi ya kata, halmashauri na manispaa.
Aidha, katika kikao kamati iliazimia kufanya tahimini ya lishe mara kwa mara ili kuhakikisha wanatoka hatua moja kwenda nyingine, kamati ikae ipitie mapendekezo yote kabla hayajaenda kwa mkuu wa mkoa, kila mjumbe katika kamati ajue na asimamie majukumu yake kikamilifu.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa