• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii

Kamati ya Ulinzi na Usalama Kukagua Miradi ya Maendeleo Kishapu

Posted on: December 2nd, 2020

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kishapu ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bi. Nyabaganga Taraba wamefanya ziara leo Desemba 2, 2020 ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.

Ziara hiyo ililenga hasa kukagua miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule za msingi zilizopo katika kata za Idukilo, Bubiki, Busangwa na Mwadui Luhumbo. Badhi ya shule hizo zilizotembelewa ni Shule ya Msingi Nyenze yenye mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu saba ya vyoo. Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu saba ya vyoo katika shule ya Msingi Idukilo. Ujenzi wa  vyumba viwili vya madarasa,  ofisi ya walimu pamoja na matundu sita ya vyoo katika shule ya msingi Bubiki B. Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu nane ya vyoo katika shule ya msingi Nyasamba na Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu saba ya vyoo katika shule yaMasagala.

Katika ziara hio Mkuu wa Wilaya ya Kishapu alizipongeza kamati za ujenzi za shule hizo kwa kazi nzuri iliyofanyika huku akiwaasa wale ambao bado hawaja kamilisha ujenzi kukamilisha mapema ili wanafunzi waanze kutumia miundimbinu hizo.

“Sisi sote katika nafasi zetu za kazi tunaiwakilisha serikali, hivyo unaposimamia mradi kama hii tufanye kwa ajili ya nchi yetu. Nawapongeza sana kwa kusimamia hii miradi vizuri kwani mmeonyesha ukomavu wa uzalendo kwa nchi yenu. Lakini pia natoa rai kwa hii miradi mingine ambayo haijakamilika, nawaongezea wiki moja mkabidhi mradi”. Amesema  Taraba

Hata hivyo katika ziara hiyo walipendekeza kuwa kamati itafanya kikao ilikufanya tathimini ya gharama zilizotumika katika ujenzi wa mirad hiyo. Aidha fedha zilizobaki kwa baadhi ya mirad izitumike kununulia mabati na mbao kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vingine vya ziada vya madarasa ambapo nguvu za wananchi zitatumika katika kukamilisha miradi hiyo.

Matangazo

  • Tangazo la kazi kada ya Afya December 12, 2018
  • Majina ya walioitwa kwenye usaili nafasi ya watendaji May 10, 2018
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • Wanafunzi Waaswa Kusoma kwa Bidii Wakizingatia Uzalendo

    January 11, 2021
  • Wachimbaji wadogo wa madini waliovamia eneo la Mgodi wa Al-Hilal watakiwa kuondoka.

    January 21, 2021
  • Milioni 42.6 kutoka mfuko wa Jimbo kuendeleza ujenzi Madarasa na Maabara.

    January 17, 2021
  • Ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kishapu kukagua mradi mkakati wa ujenzi wa vyumba vya madarasa.

    January 13, 2021
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa