Kahama Shinyanga Water Supply (KASHWASA) imekabidhi msaada wa mapipa 15 ya maji. Mapipa hayo yamekabidhiwa leo tarehe 07/05/2020 na Meneja Biashara wa KASHWASA John Zengo Ngano kwa Mku wa Wilaya ya Kishapu Nyabaganga Taraba ikiwa ni hatua ya kukabiliana na ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu unaosababishwa na Kirusi aina ya Corona.
Akizungumza Meneja huyo wakati wa kukabidhi misaada hio alisema anaunga mkono jitihada za serikali katika kutokozea Corona hivyo watu wanawe mikono mara kwa mara.
“naomba tujikinge na Corona kwa kufuata maelekezo wanayotupa wataalamu wa Afya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni. ”
Aidha, kati ya mapipa hayo Mkuu wa Wilaya amekabidhi pipa moja na barakoa 100 kwa Mkuu wa Polisi Kishapu na mengine nawili pamoja na barakoa 400 katika Gereza la Wilaya Shinyanga.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa