Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Ummy Mwalimu amesema wanafunzi wote watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022 wataanza masomo siku moja, tofauti na ilivyokuwa imezoeleka miaka ya nyuma,
Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amemhakikishia mhe, Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa wanafunzi watakao faulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani wote wataanza masomo kwa pamoja,
Mhe, Ummy amesema hayo ter 27, September 2021 jijini Dodoma katika mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Ngazi ya Taifa
Amesema amepata maagizo hayo ya Rais kupitia kwa waziri mkuu Kassim Majaliwa, kuwa mwakani anategemea kuona wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza wanaanza masomo kwa pamoja na wasisingizie uhaba wa madarasa
“mheshimiwa Rais ujumbe wako nimeupata nakuhakikishia wanafunzi wote watakao faulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wote wataanza masomo siku moja na hakutakuwa na kisingizio cha uhaba wa madarasa nakuhakikishia madarasa lazima tuyajenge na yakamilike kabla ya tar 6 january 2022. Ummy mwalimu amesema .
Pia alichukua furusa hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza sera ya elimu bila ada kwani ameshapokea bajeti yake ya miezi miwili ya mwaka 2021/2022 na wameshapeleka kwenye Halmashauri zote 84, sh 62.4 bilioni.
“Mheshimiwa Rais tunakushukuru kwani kulikuwa na uzushi kwa watu kwamba elimu bure itafutwa chini ya uongozi wako lakini kwa sasa wote ni mashahidi fedha zimeshakwenda katika halmashauri zetu kwajili ya shule zetu za misingi na sekondari”.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa