Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imeibuka kinara kikanda katika mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 baada ya kufanya vizuri katika miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama ametangaza ushindi huo Oktoba 14 katika kilele cha mbio za Mwenge Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Mhe. Mhagama alisema kuwa Kishapu imezishinda halmashauri zote za kanda iliyounda mikoa ya Tanga, Morogoro, Tabora, Iringa, Njombe, Simiyu na Shinyanga.
Katika kilele hicho ambacho kilienda sanjari na kumbukumbu ya miaka 19 ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, waziri huyo alisema kuwa mshindi atapewa kikombe, cheti na fedha taslimu sh. milioni 1.
Mirani yenye thamani ya sh. bilioni 2.2 wilayani Kishapu ilitembelewa na Mwenge wa Uhuru Agosti 20 mwaka huu ambapo Kiongozi wa mbio hizo kitaifa, Charles Kabeho aliipongeza kuitekeleza kwa ubora.
Pia aliipongeza kwa kuishirikisha jamii katika kutekeleza miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya jambo ambalo linachangia uboreshaji wa sekta hizo.
Katika maadhimisho hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein mshindi wa kitaifa alikuwa ni Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani ambaye anapata kikombe, cheti na sh. milioni 5.
Aidha, mkoa wa Geita unapewa kikombe na cheti maalumu kwa ajili ya kuwa mwenyeji wa ufunguzi huku Tanga ikipata zawadi hizo kwa kuwa mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa