Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amefanya ziara yake katika mkoa wa Shinyanga leo tarehe 03 Julai , 2020 kwa lengo la kuzindua ofisi za Ardhi na kutunuku hati za ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga.
Katika hobuba yake amesema, zaidi ya wamiliki wa ardhi laki tisa hawajamilikishwa ardhi na kupatiwa hati . Kufuatia hali hiyo Lukuvi ameagiza wamiliki wote wa ardhi ambao viwanja vyao vimepimwa waende ofisi za ardhi katika halmashauri za wilaya mkoani Shinyanga kufuatilia hati zao ili waweze kumilikishwa ardhi ndani ya siku tisini.
“Wale wamiliki wote ambao watashindwa kufuatilia hati ndani ya siku tisini wataanza kudaiwa kodi ya pango kuanzia pale mchoro ulipoidhinishwa hata kama michoro hiyo iliidhinishwa kipindi cha uhuru ataanza kudaiwa kuanzia hapo maana itakuwa ni uzembe ” amesema Lukuvi wakati wa uzinduzi huo.
Naye Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Shinyanga Ezekiel Kitilya lengo la kufungua ofisi hizo ni kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi ikiwa pia ni agizo la Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa John Pombe Magufuli ili kuimarisha utendaji kazi na uimarishaji wa usimamizi wa shughuli za ardhi.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa