Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif AliIddi amefanya ziara katika Wilaya ya Kishapu na kukagua miradi ya maendeleo.
Balozi Iddi ambaye pia ni mlezi wa Mkoa wa Shinyangana Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliwasili wilayani humoambapo alikagua mradi wa upanuzi wa kituo cha afya Kishapu.
Aliweza kujionea maendeleo ya mradi wa huounaotekelezwa kupitia fedha zilizotolewa na Serikali Kuu kwa ajili ya kuboreshasekta ya afya katika vituo mbalimbali nchini.
Alipokewa na Mkuu wa mkoa huo Mhe. Zainab Tekack naviongozi mbalimbali wa Chama na Serikali Wilaya ya Kishapu na Mkoa wa Shinyangaambako alifanya ziara.
Aidha, Balozi Iddi mbali ya kutembelea na kukaguamiradi ya maendeleo pia alipata wasaa wa kuzungumza na wananchi wa wilaya hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa