Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ametembelea Wilaya ya Kishapu.
Katika ziara hiyo ametembelea mgodi wa Almasi wa Mwadui, kuweka jiwe la msingi ujenzi wa maabara katika Shule ya sekondari Shinyanga, kuona mashine ya kuchapa maandishi ya wasioona shuleni hapo na kukagua ujenzi wa kituo cha afya Kishapu.
Mhe. Samia aliitaka Wizara ya Madini kusimamia uzalishaji wa rasilimali za madini katika mgodi huo ili kuwanufaisha Watanzania.
Alitaka timu iliyoundwa na Wizara hiyo ifike kufanya tathmini ya mapato yanayotokana na uzalishaji wa almasi ili mgodi huo uweze kulipa kodi inavyotakiwa.
Alisema tangu mgodi huo ufunguliwe umekuwa ukishindwa kulipa baadhi ya kodi kwa madai kuwa haujapata faida.
Akihutubia wananchi viwanja vya Shirecu mji mdogo wa Kishapu aliwapongeza wananchi kwa kushiriki shughuli maendeleo.
Mhe. Samia katika ziara yake aliongozana na naibu mawaziri wenye dhamana ya TAMISEMI, Ardhi, Kilimo, Madini na Ujenzi.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa