Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kupitia mfuko wa Maendeleo ya Jamii [TASAF III PHASE 1] imetoa shilingi milioni 238.9 kwa ajili ya kuziwezesha kaya masikini kwa lengo la kujikwamua kutoka katika hali duni ya maisha.
Kiasi hicho kimetolewa kuanzia Desemba 27 hadi Desemba 31, 2019 kwa ajili ya kuziwezesha kaya 5672 kutoka katika vijiji 78 viishivyo katika wilaya ya Kishapu kwa ajili ya kupeleka watoto kliniki, kuwasomesha, na miradi kama mifugo, kilimo na biashara.
Mratibu wa TASAF III wilaya ya Kishapu Sospeter Nyamhanga amebainisha kuwa lengo kubwa la TASAF ni kuzinusuru kaya masikini kwa kuwapatia ruzuku ili waweze kujikimu kwa elimu na afya.
“TASAF imelenga kunusuru kaya masikini kwa ajili ya kuwapatia watoto elimu na afya kwa ajili ya kliniki, pia katika kujikimu kiuchumi ambapo walengwa wanapewa mafunzo kupitia maafisa ugavi waliopo katika maeneo yao kuhusu kilimo bora na ufugaji wa kisasa. Tumeshuhudia wanufaika wamefanikiwa katika kilimo na kujenga nyumba zenye ubora, kufuga kuku, mbuzi, kondoo pamoja na kuanzisha biashara ndogo ndogo” Alisema Nyamhanga.
“Pia natoa wito kwa wanufaika wa ruzuku hizi kuwa wazitumie kuanzisha na kuendeleza miradi ya maendeleo kama ufugaji, kilimo na biashara bila kusahau kusomesha watoto pamoja na kuwapeleka kliniki”.
Naye Pili Ngamba ambae ni mnufaika wa TASAF III anayeishi katika kijiji cha Nhobola wilayani Kishapu ameishukuru serikali kupitia mradi wa TASAF III kwa kumwezesha kwa ajili ya kilimo ambapo amefanikiwa kuanziasha kilimo na kujenga nyumba yenye ubora.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa