• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii

MILIONI 346 KUIKARABATI MWADUI TECHNICAL.

Posted on: November 9th, 2020

Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu Sekondari kutoka Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Ndugu Benjamin N. Oganga ametembelea Shule ya Sekondari Mwadui Technical leo Novemba 9, 2020 alipokuwa anakagua ukarabati wa majengo pamoja na ujenzi wa mabweni na vyunba viwili vya madarasa ya shule hiyo. 

Shule hiyo iliyopo katika Wilaya ya Kishapu  mkoa wa Shinyanga ilianzishwa mwaka 1997 chini ya Mgodi wa Almasi wa Williamson yenye jumla ya wanafunzi  827 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne huku wanafunzi wa kike wakiwa ni 437 na wakiume 390.  Fedha kwa ajili ya ukarabati na ujenzi kutoka serikali kuu kiasi cha shilingi 226,856,239.82/= kwa ajili ya ukarabati wa majengo, Shilingi 80,000,000.00/= kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi, Shilingi 40,000,000.00/= kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.

Mkuu wa shule hiyo Ndugu Shija Dominic Kulewa ameishukuru serikali na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa kutenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo huku akiahidi kusimamia ukarahati na kukamilisha ujenzi huo.

“Nashukuru sana kwa ajili ya huu ukarabati kwani majengo ya shule hii yalikuwa yamechakaa sana, kitokana na nyufa zilizokuwepo katika madarasa ilikuwa inapelekea wanafunzi kukaa darasani kwa wasiwasi sana. Hivyo natoa pongezi za dhati kwa serikali yetu kwa kuipa elimu kipaumbele “  alisema Kulewa.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu sekondari Ndugu Oganga amepongeza maendeleo ya ujenzi huo huku akiwataka kusimamia kwa umakini ujenzi huo ili majengo yawe imara huku akishauri fedha zinazibaki zitumike kupaka rangi na kuweka bati mpya kwenye majengo mengine.

“nataka mwenge ujao utakapopita hapa pawe mfano kwa maana ya ubora wa majengo. Pia fedha zitakazobaki kutokana na ujenzi huu zitumike kukupaka rangi majengo mengine ili yawe ya kufanana na haya yaliyorekebishwa “  alisema Oganga.

Matangazo

  • Tangazo la kazi kada ya Afya December 12, 2018
  • Majina ya walioitwa kwenye usaili nafasi ya watendaji May 10, 2018
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • Wanafunzi Waaswa Kusoma kwa Bidii Wakizingatia Uzalendo

    January 11, 2021
  • Wachimbaji wadogo wa madini waliovamia eneo la Mgodi wa Al-Hilal watakiwa kuondoka.

    January 21, 2021
  • Milioni 42.6 kutoka mfuko wa Jimbo kuendeleza ujenzi Madarasa na Maabara.

    January 17, 2021
  • Ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kishapu kukagua mradi mkakati wa ujenzi wa vyumba vya madarasa.

    January 13, 2021
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa