Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Boniphace Nyangindu Butondo amewapongeza wananchi kwa nguvu kazi na michango ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara Wilayani Kishapu.
Mhe. Butondo ameyasema hayo alipokuwa na ziara yake ya siku mbili Jimboni humo ambapo alizindua mfuko wa Jimbo na kutambulisha kikao cha kwanza kupitia mwenyekiti wa wa mfuko huo.
Kikao hicho kiliazimia kutoa fadha kwa ajili kuunga mkono miradi ya maendeleo iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi hasa vyumba vya madarasa na maabara kwa lengo la kutekeleza agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Mjaliwa la kuongeza vyumba vya madarasa ili ifikapo Februari 2021 wanafunzi wapate mazigira mazuri ya kujisomea.
Katika ziara yake alitembelea tarafa za Mondo, Negezi na Kishapu ambapo jumla ya miradi ya maendeleo 15 imenufaika na mfuko huo wa Jimbo huku jumla ya kiasi cha fedha shilingi milioni 42.6 kilitolewa na Mbunge huyo kupitia mfuko wa jimbo kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo ukiwemo na mradi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Polisi Wilaya ya Kishapu unaojengwa kwa nguvu za wananchi.
“Fedha hizi zitaenda kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na maabara ulioanzishwa kwa nguvu za wananchi ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari” alisema Butondo.
Mhe. Butondo ameendelea kuwashukuru na kuwapongeza wananchi wa Jimbo la Kishapu kwa kuwachagua kwa kishindo katika uchaguzi mkuu iliopita wa Rais, wabunge na Madiwani na kuahidi kuwatumikia kwa nguvu zote.
“Wananchi wa Kishapu mliniamini mkanichagua ili tufanye maendeleo naomba tushirikiane ili kwa umoja wetu tuwezek uleta maendeleo katika Jimbo letu, naomba tuzidi kushikana mkono hasa katika mradi mkakati huu wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara ili watoto wetu wapate elimu kwenye mazingira rafiki” aliongeza Butondo.
Aidha Mbunge huyo aliwaasa viongozi wa ngazi zote kuanzia kata, vijiji na vitongoji kusoma taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi wao kupitia vikao na mikutano ya hadhara kwani kufanya hivyo kutawajengea uaminigu kwa wananchi wao.
Katika ziara hiyo amesisitiza pia suala zima la usimamizi wa thamani ya fedha kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuwataka wataalamu ngazi ya Halmashauri kusimamia ujenzi huo ili uwe katika kiwango kinachitakiwa na kudumu kwa muda mrefu.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa