Naibu Waziri Ofisi Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe, Anthony Mavunde amesema vijana wilayani Kishapu watanufaika na kilimo cha mboga mboga kupitia mradi wa kitalu nyumba (green house) unaotarajiwa kutekelezwa.
Mhe. Mavunde amesema hayo Septemba 19, 2018 wilayani Kishapu wakati akikagua miradi ya vijana ikiwemo uandaaji wa maeneo ya vitalu kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa kuchangmkia fursa ya kutenga eneo kwa ajili ya kitalu nyumba ambacho kitatumika kufundisha vijana kilimo cha chenye tija.
Naibu Waziri huyo alisema kuwa kupitia programu hiyo ya kilimo vitalu nyumba wanaunga mkono Serikali katika kukuza uchumi wa viwanda ambapo.
“Kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana tumeona tuwasaidie kununua mashine ndogo ndogo waweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo, kwa hiyo hakuna haja nyanya yako kuharibika unaweza kuisindika mwenyewe,” alisema.
Mavunde aliongeza kuwa mradi huo ukishika kasi vijana watajifunza na kuwa na uwezo wa kujitengenezea vitalu vyao na kuvisambaza kwa wengine na hivyo kutengeneza ajira.
Aidha, Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo Shirika la REDESO/OXFAM imejenga kitalu nyumnba kupitia kikundi cha Mwanga kilichopo kijiji cha Unyanyembe chenye thamani ya sh. milioni 2.96.
Pia imejenga kisima kwa ajili ya kuwezesha shughuli za umwagiliaji wa mazao yatakayopandwa kwenye kitalu nyuma hicho, kisima pamoja na vifaa vimegharimu sh. milipni 3.
Tayari kimeandaliwa na mbegu za nyanya (tomato milele F1) zipandwe katika kitalu nyumba hicho.
Aidha, alitoa rai kwa mikoa mingine iliyobaki kuandaa maeneo kwa ajili ya vitalu nyumba kama ambavyo viongozi wa kitaifa walivyoagiza kwa nyakati tofauti.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa