Na Ofisi ya Habari, Kishapu
Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 umepokelewa kimkoa kijiji cha Kinampanda kata ya Shagihilu katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kutoka Simiyu na kuzindua miradi ya maendeleo yenye thamani ya sh. bilioni 3.7.
Katika mapokezi hayo Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini alimkabidhi mwenzake wa Shinyanga, Albert Msovela ambaye alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kishapu.
Katika mbio hizo jumla ya miradi 12 ilizinduliwa ikiwemo ya kituo cha mafuta wenye thamani ya sh. milioni 337 kutoka kwa mjasiliamali Kija Ng’wani na mashine ya kusindika mafuta ya alizeti na unga wa mahindi sh. 244.
Mingine ni mashine ya kukoboa mpunga na kuweka katika madaraja sh. milioni 535.8 na ufugaji ng’ombe sh. milioni 400 ya mjasiliamli Mabela Masolwa pamoja na eneo la viwanda lenye ekari 278 ambao thamani yake ni sh. bilioni 1.1.
Mradi wa ujenzi wa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria sh. milioni 755 uliofadhiliwa na shirika la Investing in Children and their Society (ICS), nyumba za walimu sh. milioni 55.8 uliofadhiliwa na mgodi wa Mwadui.
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu iligharamia mradi wa pikipiki kwa vijana wajasiliamali wenye thamani y ash. Milioni 21, hudni zenye thamani y ash. Milioni 10.5 kwa wanawake wajasiliamali na utengenezaji bidhaa za ngozi wa Badimi sh. milioni 20.
Akizungumza wakati wa mbio hizo, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Amour Hamad Amour aliwataka Watanzania bila kujali tofauti zao kuuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kulinda rasilimali zilizopo nchini.
Alisema taifa litaongozwa kwa kufanya kazi kwa bidii ili tufikie malengo na maendeleo huku akiongeza kuwa tumezunguzkwa na mito na ardhi yenye rutuba ya hivyo wananchi wajitume.
Alipongeza wilaya kwa kuhakikisha inakuwa na viwanda huku akiwataka wananchi kutumia bidhaa zinazozalishwa wilayani badala yake kuwa tegemezi kwa bidhaa za kutoka nje ya nchi ili kukuza uchumi wa taifa.
Amour aliasa miradi inayozinduliwa na Mwenge iwaguse wananchi na waisimamie ili kuleta tija na ufanisi huku akipongeza pia kwa mapambano dhidi ya Ukimwi na rushwa.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa