Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angelina Mabula amefanya ziara katika wilaya ya Kishapu leo tarehe 17 August 2020 kwa lengo la kukagua utekelezaji wa kazi sekta ya Ardhi, Miradi ya Shirika la Nyumba (NHC), kuzungumza na watumishi pamoja na kugawa Hati Miliki kwa wananchi wa wilaya ya Kishapu.
Sekta ya Ardhi katika Wilaya ya Kishapu inafanya kazi ya Uthamini, Mipango miji, Upimaji wa Ramani pamoja na Ardhi tawala na Usimamizi. Aidha katika utekelezaji wake za kazi, sekta ya Ardhi inafanya kazi sambamba na na ujenzi wa Nyumba za Bei nafuu za Sgirika La Nyumba La Taifa (NHC), umilikishaji wa viwanja ambapo Halmashauri imefanikiwa kuandaa michoro ya Mipango Miji 24 yenye jumla ya viwanja 5848 vya matumizi mbalimbali ambapo kati ya hivyo vilivyopimwa ni 2853. Ukusanyaji wa Kodi ya Pango la Ardhi, pamja na urasimishaji wa makazi holela.
Naye Naibu wa arhdi ameitaka halmashauri kuhakikisha maeneo yote ya umma yanapimwa na kuyamilikisha ili kukwepa migogoro na wananchi.
“tunasisitiza upimaji wa maeneo ya umma ili kukwepa migogoro na migongao na wananchi, usipopima na kulitambua eneo lako tegemea migogoro isiyoisha, maeneo yote ya taasisi za umma. Nahitaji kupata taarifa ya hii kazi ”
Aidha katika ziara hio Naibu Waziri wa Ardhi amewataka kitengo cha Ardhi katika halmashauri kufanya kazi kwa weledi wakishirikiana na ofisi za Ardhi mkoa huku akiwapongeza kwa kuwa na idadi kubwa ya maeneo yaliyopimwa katika wilaya ya Kishapu.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa