• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii

OPE yafanya Tathimini juu ya Mimba na Ndoa za Utotoni

Posted on: February 4th, 2021

Shirika la OPE (Organization of People Empowement) wamefanya tathimini juu ya Mradi wa Kutokomeza mimba na ndoa za utotoni katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu leo Februari 4, 2021.

Mradi huo unaotekelezwa katika kata ya Busangwa wilayani Kishapu ulianza mwaka 2015 ukiwa na lengo la kuijengea jamii uelewa wa kutambua mila kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni kupitia mikutano ya hadhara kutoa elimu kwa  wanajamii kupinga mila potofu zinazochangia mimba na ndoa za utotoni.

Akifungua kikao hicho cha Tathimini Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Ndugu. Joseph Swalala amesema kuwa jamii inayotuzunguka inahitaji elimu ya kutosha juu ya masuala haya hivyo amewaomba shirika la OPE kuendelea kuielimisha jamii juu ya masuala ya kupinga mimba na ndoa za utotoni.

“Nawaomba Shirika la OPE kuendelea na harakati hizi za kuoa elimu kwa jamii juu ya mila kandamizi zinazopelekea mimba na ndoa za utotoni kwa kushirikiana na Maafisa Maendeleo ya Jamii Kata” amesema Swalala.

Akitoa tathimini hiyo Afisa Miradi wa Shirika la OPE, Joseph Kasya amesema kupitia mradi wa Kutokomeza Mimba na Ndoa za Utotoni chini ya Shirika la OPE kuna mafanikio makubwa kwani jamii inatoa taarifa na ushahidi juu ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili kwa watoto pamoja na mimba na ndoa za utotoni. Aidha wazazi na walezi wamepata uelewa mzuri wa malezi ya watoto wao hivyo kupelekea kupungua kwa mimba na ndoa za utotoni.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa OPE, William Pius Shayo amewataka wazazi na walezi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na dawati la jinsia kuhakikisha kwa pamoja wanasimama kuwalinda watoto ili kuepuka kukatisha ndoto na malengo yao.

“Sisi kama jamii tuna wajibu mkubwa wa kuhakikisha watoto wetu wanatimiza ndoto zao kwa kupinga mila kandamizi zinazopelekea mimba na ndoa za utotoni hivyo tuendelee kushirikiana kwa pamoja kutekeleza hilo. Pia natoa shukrani zangu kwa ofisi ya mkurugenzi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na dawati la jinsia kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kutupatia” amesema Shayo.

Akihitimisha kikao hicho cha tathimini Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu amepongeza Shirika la OPE kwa kazi wanayoifanya ya kuhakikisha mimba na ndoa za utotoni katika wilaya yetu zinatoweka na kusisitiza walezi na Afisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya kata kufuatilia maendeleo ya ‘clubs’ mashuleni ili kuwapa elimu juu ya madhara ya mimba na ndoa za utotoni.

Mkurugenzi Mtendaji wa OPE, William Pius Shayo akielezea jambo wakati wa tathimini ya kupinga mimba na ndoa za utotoni katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu


Afisa Miradi wa Shirika la OPE, Joseph Kasya akitoa tathimini juu ya Mradi wa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni

Matangazo

  • Tangazo la kazi kada ya Afya December 12, 2018
  • Majina ya walioitwa kwenye usaili nafasi ya watendaji May 10, 2018
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • OPE yafanya Tathimini juu ya Mimba na Ndoa za Utotoni

    February 04, 2021
  • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango kukagua Miradi ya Maendeleo

    February 02, 2021
  • Milioni 34.4 kunufaisha Vikundi vya Ujasiriamali Kushapu

    January 18, 2021
  • Wanafunzi Waaswa Kusoma kwa Bidii Wakizingatia Uzalendo

    January 11, 2021
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa