Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack Septemba 18 ametembelea na kukagua mradi wa upanuzi wa kituo cha afya Kishapu ulioanza kutekelezwa katika Wilaya ya Kishapu.
Akiwa katika mradi huo kituoni hapo wenye thamani ya sh. milioni 400 Mhe. Telack alitaka nguvu za wananchi zishirikishwe katika ujenzi wa vituo vya afya.
Sanjari na hilo aliwataka wataalamu waziache kamati za ujenzi zifanye kazi ya kusimamia miradi hiyo ya ujenzi wa vituo vya afya.
“Wataalamu msiingilie hizo kamati na tunachotaka ni majengo imara, tofali imara, simenti iwe haijaexpire (haijakwisha muda wake), agizeni kwa bei ya jumla na nafuu itatusaidie kujenga kituo,” alisisitiza.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa alikutana na Kamati ya Lishe Wilaya ya Kishapu na kuwataka wataalamu hao kutoa elimu ya lishe kwa wananchi ili kuondoa udumavu.
Aliagiza fedha zinazotengwa kwenye bajeti kwa ajili ya masuala ya lishe zisimamiwe vizuri ili kuhakikisha zinafanya kazi hiyo lishe.
“Kila mtu kwa nafasi yake akifanya kile kinachotakiwa kufanyika mkoa wetu utasimama vizuri ka hiyo kila mmoja kwa jukumu lake,” alisisitiza Mhe Telack.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa