Redeso kwa kushirikiana na Oxfam Tanzania leo wamekabidhi msaada wa vifaa kinga kwa ajili ya kujikinga na Covid-19. Msaada huo umetolewa leo tarehe 16 June 2020 katika Kituo cha Afya Kishapu ambacho kimetengwa maalumu kwa ajili ya wagonjwa wa Corona.
Mratibu wa Miradi ya Oxfam Kanda ya Ziwa Vilentine Shipula amekabidhi vifaa kinga hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bi, Nyabaganga Taraba vyenye thamani ya shilingi 29,579,000/= ambavyo ni Personal Protective Equipment (PPE) 205, SURGICAL Face Masks 970, Face Masks (N95) 1200, chupa 11 za Sodium Dichloroisocyanurete kila moja ina jumla ya pic 100.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mratibu wa Miradi wa Oxfam Tanzania amesema Oxfam inaunga mkono jitihada za Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Pombe Maguful katika harakati za kukabiliana na ugonjwa wa Corona.
“Lengo kuu la mradi huu ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na janga la Corona hivyo vifaa hivi mkavitumie vizuri na kuvitunza katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona ” alisema Shipula.
Naye Meneja Miradi wa Redeso Kishapu Charles Buregea wakati wa kukabidhi mdaada wa vifaa tiba amesema kwa kuwa Redeso iko kwenye eneo husika la Mradi wa kukabiliana na Maafa hivyo kwa kushirikiana na Oxfam wametoa msaada wenye thamani ya shilingi 7,000,000/=
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kishapu wakati wa kupokea msaada huo wa vifaa tiba amewashukuru Redeso na Oxfam kwa kuchangia jitihada za kujikinga dhidi ya corona. Aidha aliwashukuru wananchi, wafanyakazi na wauguzi kwa kushirikiana kujikinga dhidi ya Corona huku akiwasihi kiendelea kujikinga dhidi ya Corona.
Katika hali hiyo, wilaya ya Kishapu hadi sasa haina mgonjwa wa Corona,tuzidi kujikinga dhidi ya Corona.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa