Serikali imehimiza uchakati na usindikaji wa bidhaa za kilimo ili kuongeza tija, kutoa ajira na kuboresha maisha ya Watanzania.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe, Anthony wakati alipofanya ziara ya kikazi wilayani Kishapu.
Mhe. Mavunde alisema lengo la Serikali ni kuwafanya vijana wengi zaidi wachangie nguvu kazi kwenye uchumi wa viwanda na kuwa ifikapo mwaka 2025 asilimia zaidi ya 40 ya vijana wawe wamejiari kwenye viwanda.
Alifafanua katika lengo hilo mambo matatu yafanyike yakiwemo vijana wajishughulishe na kilimo chenye tija, wafundishwe namna ya kutengeneza vitalu nyumba (green house) vitakavyotumika kulima mazao.
Naibu waziri alisema kwa upande wa Serikali itaendelea kukopesha vijana kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambapo hadi sasa vimekopeshwa vikundi takriban 755 zaidi ya sh. bilioni 4.5 huku akihimiza vikundi vitakavyohitaji mikopo viwe vimesajiliwa.
Awali akiwasilisha taarifa ya wilaya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, George Kessy alisema kuwa wilaya imeendelea kufanya jitihada za uanzishwaji wa nyumba kitalu ambayo tayari imetengewa eneo kwa ajili ya miundombinu ya maji.
Alisema eneo hilo litatumika kama shamba darasa kwa vikundi vya vijana kutoka sehemu mbalimbali wilayani Kishapu Ili kuwajengea uwezo wa kuzalisha mazao na kuongeza kipato chao hivyo kukuza uchumi.
Kwa kushirikiana na wadau alisema halmashauri imebaini jumla ya vijana wajasiliamali 1,215 ambapo kati yao 705 ni wanaume na 501 ni wanawake wakijishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo bodaboda, uchimbaji mdogo, biashara na ushonaji.
Kaimu mkurugenzi mtendaji huyo aliongeza kuwa Imetoa mafunzo ya ujasiliamali, kilimo na ugufahi bora kwa vijana 463 ambao 268 ni wanaume na 195 ni wanawake.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa