Wanafunzi wa shule za msingi katika Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wamepatiwa elimu ya afya ya kinywa na meno na kufanyiwa uchunguzi.
Elimu hiyo imetolewa leo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani yaliyofanyika kimkoa wilayani humo.
Miongoni mwa shule zilizotembelewa na wataalamu wa afya ni Isoso, Mhunze, Mlimani na Buduhe.
Mtaalamu wa afya Anold Shirima kutoka Kishapu alisema ni wamegawa miswaki, dawa za meno na vipeperushi vyenye ujumbe ili kuwapa elimu wanafunzi.
Mbali ya kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pia mtaalamu wa afya wa Mkoa, Nuru Mpuya pia alikuwepo.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa