Elimu ya afya juu ya kujikinga na ugonjwa wa Homa ya Mapafu unaosababishwa na Kirusi aina ya Corona (COVID-19) imetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kupitia Timu ya Majanga ya Afya Wilayani humo. Elimu hio imetolewa kwa kwa wafanya biashara pamoja na wana jamii wote wakiwemo leo tarehe 19 March 2020 katika Mnada wa Mhunze wilaya Kishapu mkoani Shinyanga.
Katika hatua ya kukabiliana na ugonjwa huo, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Nyabaganga Taraba alijumuika pamoja na Timu ya Afya ya Hospitali ya Jakaya Mrisho Kikwete na wafanyakazi wa Halmashauri katika Wilaya ya Kishapu wakifanya zoezi hilo kwa vitendo kwa kunawisha watu mikono kwa kutumia ‘Hand Sanitizers’ ambayo ni mchanganyiko wa ‘spirit na glycerine’.
Aidha katika harakati hizo wafanya biashara walikumbushwa kuwa katika hali ya usafi huku wakielezewa namna ya kuengeneza Hand Sanitizers, dalili kuu za COVID-19 na jinsi ya kujikinga.
kutokana na mwingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi tunapaswa kuchukua tahadhari hasa kwa watu wenye dalili za ugonjwa huu kama vile matatizo katika mfumo wa hewa ikiambatana na homa kali, kukohoa, vidonda kooni, kubanwa mbavu, mwili kuchoka, maumivu ya misuli na mafua makali. Ambapo inaaminika dalili za ugonjwa huonekana siku 1-14 baada ya mtu kuambukizwa.
Kuimarisha usafi kwa kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni mara kwa mara au kutumia hand sanitizers kwa kuchanganya glycerine na spirit,ambapo kwa ujazo wa lita moja ya spirit unaweka vifuniko viwili vya glycerine, funika mdomo na pua wakati wote wa kukohoa au kupiga chafya. Kwa kuwa virusi vya ‘Covid2019’ vina ukubwa wa 400-500 Micro hivyo kwa kutumia kitambaa au mikono safi unaweza kuzuia virusi hivi, kuepuka kugusana na mwenye dalili za Corona, kutupa vifaa vilivyotumika kama masks na hand sanitizers katika chombo cha kuhifadhia taka, kusafisha kwa kutumia dawa ya kuua vijidudu kwenye vitasa vya milango, sakafu na nguo za wagonjwa, epuka kugusa pua, macho na mdomo kwa mikono isiyo safi, kuepuka kuwa karibu sana na watu wenye Corona, hizi zitachangia kwa kiasi kikubwa kuepuka ugonjwa wa Corona.
Hadi sasa kwa Tanzania jumla ya wagonjwa wa COVID-19 ni 8 ambapo sita kati yao ni raia wa Tanzania na wengine wawili ni raia wa kigeni ambapo ugonjwa huu kwa Tanzania haujaripotiwa kuua mtu hata mmoja. Katika juhudi za kudhibiti kuenea kwa maambukizi wageni wote wanaoingia nchini kutoka katika mataifa yaliyoripotiwa kuwa na ugonjwa huo watatengwa kwa siku 14. Aidha agizo hilo lililotolewa na Raisi wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania,John Pombe Magufuli linawajumuisha Watanzania wanaorejea nyumbani kutoka nchi nyingine.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa