Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umefanya kikao cha kujadili mfumo wa ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma (PEST) katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Katika kikao hicho umekutanisha watendaji wa kata, maafisa Kilimo, Afya na Maendeleo ya Jamii kutoka Halamahauri hiyo pamoja, madiwani pamoja na wadau kutoka vituo vya taarifa na maarifa.
Mhamasishaji kutoka TGNP, Hancy Obote alisema mtandao huo unafanya kazi katika Halmashauri hiyo ambapo imekuwa ikiijengea jamii kutambua wajibu wao katika maendeleo.
Alisema mfumo huo unafuatilia ufanisi na uwajibikaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata za Kishapu pamoja na kuweka sawa jamii kuhusu masuala yanayohusu sheria.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa