Mkuu wa wilaya ya Kishapu mhe Joseph Mkude amewataka viongozi wote kuanzia vijiji mpaka kata mikutano ya mkuu wa wilaya kudhuria ni lazima, ameyazungumza hayo akiwa anazungumza na wananchi wa kata ya kishapu nakuomba viongozi wote kuanzia kijiji mpaka kata kwenye ziara za mkuu wa wilaya anapokuwepo kata husika ni lazima uongozi wote wa kata uwepo kwa sababu katika jamii kuna changamoto nyingi ambazo zinawalenga viongozi hao ,
Mhe, Mkude alisema kuna baadhi ya watendaji wanakwepa kuhudhuria mikutano ya mkuu wa wilaya kwa sababu wanakuwa na changamoyo nyingi sana katika vijiji vyao hivyo kuogopa kuja kujibu tuhuma zinazokuwa zinawakabili kwenye jamii zao
“watendaji wote wa vijiji, mtendaji wa kata, polisi kata, afisa maendeleo kata n.k ukisikia nina ziara kwenye kata yako, kama huna sababu ya msingi inayotambulika kuhudhuria kikao cha mkuu wa wilaya ni lazima baadhi ya maeneo nimekuwa nikipita kata ina vijiji 5 lakini mtendaji wa kijiji amehudhuria mmoja, au afisa maendeleo hahudhurii, pengine hata mtendaji wa kata hayupo kwa kweli hiyo hali sitaivumilia kabisa na hatutabembelezana, na ukiona kiongozi anakimbia majukumu jua anashida kubwa kwa wananchi, kwa hiyo niwaombe mtatue changamoto za wananchi, changamoto ni nyingi sana, sasa msipo wajibika nyie haina maana ya kuwatumikia wananchi, ni lazima kila kiongozi awajibike kwa nafasi yake” pia aliongezea kwa kusema “watendaji wengi wa kijiji hawasomi mapato na matumizi kwa wananchi”
Abdalah lomole mkazi wa kijiji cha mhunze kata ya kishapu amempongeza mkuu wa wilaya kwa kuliona hilo kwani viongozi wengi wamekuwa wakikwepa majukumu yao katika kutenda haki kwa wananchi
“namshukuru sana mkuu wa wilaya hakika tumepata mpambanaji wa kutupambania wilaya yetu , ni kweli kabisa baadhi ya viongozi hawawajibiki kama inavyotakiwa kuwajibika, kwani wamekuwa wababaishaji sana, hata mikutano ya hadhara hawaaliki, hivyo inapelekea ugumu kwetu hata kutambua tu mapato na matumizi, namuomba mkuu kwa viongozi wazembe asisite kuwaajibisha hili litatusaidia hata kuleta maendeleo kwenye wilaya yetu kazi iendelee………….”
Annastazia Christopher katibu wa sungusungu kijiji cha isoso kata ya kishapu, vilevile amepongeza maamzi ya mkuu wa wilaya ya mhe, Mkude kuwataka viongozi kuhudhuria vikao vya mkuu wa wilaya kwa sababu hii itaongeza ufanisi katika utendaji kazi na viongozi watafanya kazi kwa weledi mkubwa sana
“Mkuu wetu wa wilaya kwa kweli yupo sahihi kabisa, hawa viongozi wenzangu baadhi huwa hawaji kwenye vikao wakiogopa maswali kwa wananchi kwa sababu hawana uhakika na kazi zao wanazo zifanya, kutokana na maamzi aliyoyachukua mkuu ni sahihi na nina muunga mkono kwa sababu hawa viongozi wakifata yale wanayotakiwa kuyafanya itakuwa vizuri mno na utendaji kazi wao utakuwa mzuri na wenye weledi mkubwa na sisi tupo tayali kumsaidia mkuu wetu kupambna na viongozi wanaokwamisha maendeleo ya wilaya yetu”
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa