Wajumbewa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Shinyanga wamefanyaziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Wilaya ya Sengerema jijiniMwanza kujifunza namna ilivyofanikiwa katika miradi ya maendeleo.
Miradiiliyotembelewa na wajumbe hao ni pamoja na urasimishaji na upimaji wa ardhi manispaaya Ilemela pamoja na mradi wa maji ya Ziwa Victoria katika Halmashauri ya Wilayaya Sengerema.
Ziarahiyo ilihusisha wajumbe wa ALAT kutoka Halmashauri za Wilaya za Kishapu, UshetuMsalala, Shinyanga, Mji wa Kahama na Manispaa ya Shinyanga pamoja na baadhi ya wataalamuwake.
Katikakikao kilichowakutanisha wataalamu wa Ardhi na ujumbe huo kutoka mkoaniShinyanga walipata taarifa kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na idarahiyo ambazo zimesaidia kutatua migogoro ya ardhi.
Akielezeakuhusu miradi hiyo, Afisa Mipango Miji Manispaa ya Ilemela, Shukrani Kyando alisemakatika mwaka uliopita walipanga kupima viwanja 16,000 na hadi sasa wamepima 33,200huku matarajio ni kufikia 52,000.
Alisemahadi sasa tayari wana michoro ya viwanja 52,000 ambapo wanaandaa michoro yamipango miji baada ya kuchukua taarifa za kila nyumba ili kuweza kuwa na mjiuliopangika vizuri.
Kwa upandewao baadhi ya wananchi kutoka Kata ya Shibuda kuwa mradi wa urasimishaji waardhi wameupokea vizuri na kueleza kuwa umeweza kuondoa migogoro ya ardhi.
Wakishukuruna kupongeza Idara ya Ardhi katika manispaa hiyo, wananchi hao walisemawamepimiwa vizuri viwanja kupitia upimaji shirikishi ambao umefanyika bila kuharibumipango miji.
Akitoamaoni kuhusu mradi huo Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Shinyanga, Ngasa Mbojealiupongeza na kusema kuwa hilo ni jambo zuri na linalofaa kuigwa nahalmashauri za mkoa huo.
Alibainishakuwa wao kama wajumbe wa ALAT Mkoa wa Shinyanga wanayo mengi ya kujifunzakutoka katika mradi huo wa upimaji ardhi unaotekelezwa na Halmashauri ya Manispaaya Ilemela.
“Tumeonatujifunze kutoka kwa wenzetu hawa wa Ilemela na na ni jambo zuri kwani unapimakulingana na eneo lilivyo na sisi kule kwetu (Shinyanga) tuna miji iliyoanzakupanga kwa mfano kule Mhunze (Wilaya ya Kishapu) na Old Shinyanga (Manispaa),”alidokeza Mboje.
Wakiwawilayani Sengerema wajumbe hao walitembelea mradi wa maji ya Ziwa Victoria nakujionea shughuli za uzalishaji maji kutoka chanzo hicho na kuyasambaza mji waSengerema.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa