• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii

Wanafunzi Waaswa Kusoma kwa Bidii Wakizingatia Uzalendo

Posted on: January 11th, 2021

Naibu Katibu Mkuu wa Elimu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Gerald Mweli, amesema Wanafunzi wa kidato cha Nne na Sita, muda wao walionao kwa sasa ni miezi Minne kwa kidato cha Sita na Miezi tisa kwa kidato cha Nne kuamua hatma ya maisha yao kielimu na mafanikio yao kimaisha.

 Mweli aliyazungumza hayo wakati wa ziara yake ya kikazi leo Januari 11, 2021 wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

“Muda mlionao ninyi ni mchache sana wa kuamua hatma ya maisha yenu kielimu, kuna wenzenu walifukuzwa shule huko mkoani Arusha juma moja kabla ya kuanza mitihani yao ya kuhitimu baada ya nidhamu yao kwenda kinyume na sheria, taratibu na kanuni za elimu kwa kuharibu miundombinu ya shule.” alisema Mweli.

Naibu Waziri huyo amezidi kusisitiza kuwa tabia zote mbaya zinazoenda kinyume utaratibu wa elimu kama kuvuta bangi, utoro, wizi  na kuharibu miundombinu ya shule ni baadhi ya makosa ambayo yataweza kuwafukuzisha shule hata kama wamebakiza siku mbili kuanza mitihani yao, hivyo akawaasa wawe wanafunzi watiifu.

Mweli amewaonya wanafunzi hao kuwa, endapo watashindwa kuzingatia nidhamu wakiwa shuleni hapo, basi ipo siku watafunzwa nidhamu wakiwa chini ya miongozo ya vyombo vya dola vya polisi na Magereza, “Sitaki kuona vijana wangu, wadogo zangu mnafikia huko”.

“Kidato cha sita tambueni mna miezi minne tu ya kuamua hatma yenu, na ninyi kidato cha Nne mna miezi Tisa tu, hivyo ni hiyari yenu kuamua nini mnakihitaji katika Maisha yenu siku zijazo, ni wazi kwamba, kusoma sio kibali cha kutajirika, lakini itakusadia kwa kiasi fulani kuyafikia malengo yako na kukujengea heshima mbele ya jamii yako.” Mweli amewasisitiza wanafunzi hao.

Awali akitoa taarifa ya Shule ya Sekondari Shinyanga, mbele ya Naibu Katibu Mkuu, Mkuu wa Shule hiyo Benard Ishengoma, amemwambia Naibu Katibu Mkuu kuwa, Shule ya Sekondari Shinyanga ilipokea kiasi cha Shilingi 897,335,247.05 kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo kongwe yenye zaidi ya miaka 55 toka kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1966.

Akiwa shuleni hapo, Naibu Katibu Mkuu, amewakumbusha walimu majukumu yao lakini pia, kuwataka kuwasimamia wanafunzi na kuwahimiza kujiunga na Klabu mbalimbali ikiwepo Skauti, lakini pia kuwakumbusha kuzingatia suala la uzalendo ikiwepo kuwafundisha wanafunzi nyimbo za kizalendo ikiwepo, Wimbo wa Taifa, Wimbo wa Afrika Mashariki sambamba na Wimbo wa Uzalendo wa Tanzania nakupenda kwa moyo wote, kila mara.

Naibu Katibu Mkuu Gerald mweli amefika shuleni hapo ikiwa ni sehemu ya ziara yake, ambapo mbali ya kutembelea shule ya Sekondari Shinyanga ametembelea na kukagua, Shule ya Sekondari Mwadui ufundi na Shule ya Sekondari Maganzo na kisha kufanya mkutano wa pamoja na Waratibu Elimu Kata, Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu kutoka shule mbalimbali wilayani Kishapu.

Matangazo

  • Tangazo la kazi kada ya Afya December 12, 2018
  • Majina ya walioitwa kwenye usaili nafasi ya watendaji May 10, 2018
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • OPE yafanya Tathimini juu ya Mimba na Ndoa za Utotoni

    February 04, 2021
  • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango kukagua Miradi ya Maendeleo

    February 02, 2021
  • Milioni 34.4 kunufaisha Vikundi vya Ujasiriamali Kushapu

    January 18, 2021
  • Wanafunzi Waaswa Kusoma kwa Bidii Wakizingatia Uzalendo

    January 11, 2021
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa