Shirika la Kivulini pamoja na Redeso wamefanya kikao kuweka mikakati ya kuboresha mfumo wa rufaa kwa wahanga wa ukatili kipindi cha mlipuko wa magonjwa.
Shirika la Kivulini linalojihusisha na masuala ya Haki za Wanawake yenye dhima ya “Jamii salama, Familia salama’na Redeso (Relief for Development Societies) leo tarehe 22 Mei 2020 wamejadili mambo yanayo wakandamiza akina mama na watoto hasa katika kipindi hiki cha janga la Corona.
Haya yamesemwa na Afisa Tathimini na Ufuatiliaji kutoka Kivulini Godfrey Paschal “Kutokana na utafiti mdogo uliofanywa na Kivulini katika kata tatu wilayani Kishapu ambazo ni Ngofila, Itilima na Kiloleli imebainika kuwa watoto wanatumika kama wazalishaji katika kujipatia kipato cha familia, wana jamii wengi wanasema hawana taarifa sahihi juu ya ugonjwa wa Corona hivyo kuwaweka katika hatari ya maambkizi, kuyumba kwa biashara kwa akina mama hivyo kuongezeka kwa ukatili katika familia zao, Wahanga wa ukatili hawaendi kutafuta kwa watoa huduma hususani wale ambao wako nje ya kijiji kama vile polisi, maafisa ustawi kwa sababu ya uhitaji wa barakoa na wanadai kwenye kijiji hakuna barakoa wala vifaa vingine vya kujikinga”
Katika kikao hicho wajumbe walitoa mapendekezo ya namna ya kuboresha utoaji huduma kwa wahanga wa ukatili kama vile, kusogeza huduma kwa wahanga wa ukatili ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo, kuendelea kutoa elimu kwa njia mbalimbali kwa jamii juu ya ukatili katika kipindi hiki cha janga la Corona, timu za kukabiliana na majanga zilizoundwa vijijini zipewe posho kwa ajili ya kujikimu ili kurahisisha zoezi la kutoa elimu, watendaji waripoti kwenye vyombo vya usalama masuala ya ukatili na mimba kwa wanafunzi katika kipindi hiki cha Corona. Watendaji wa kata watoe maagizo kwa watendaji wa vijiji kuzuia watoto kujihusisha na shughuli za kujipatia kipato nje ya familia, pindi shule zitakapofunguliwa wanafunzi wapimwe mimba na walimu wazingatie mahudhurio ya watoto shuleni, shuleni ziunde kamati ndigi kutoa elimu juu ya ukatili kwa watoto na haki zao ili kutokomeza ukatili majumbani na kwenye jamii.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa