Watoto 53,911 wa umri wa chini ya miaka mitano wamesajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa wilayani Kishapu.
Takwimu hizo zimetolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya hiyo, Joseph Swalala.
Alisema zoezi hilo limefanikiwa kwa kiwango cha asilimia 95 ya lengo lililowekwa.
Swalala aliongeza kuwwa zoezi hilo linalofanyika katika vituo 84 wilayani humo limelenga kuwafikia watoto 55,233.
Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA) unaratibu zoezi hilo katika wilaya za mikoa mbalimbali sanjari na kuwaingiza kwenye mfumo.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa