Hospitali ya Jakaya Mrisho Kikwete katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imefanya kliniki tembezi ambapo madaktari bingwa kutoka katika hospitali mbalimbali wamejumuika pamoja na madaktati katika hospitali hio kufanikisha huduma ya kliniki tembezi. Katika kliniki hio wagojnwa wenye matatizo ya uzazi na yale ya upasuaji walipata matibabu ya kibingwa.
Huduma ya kliniki tembezi imefanyika kwa siku 10 kuanzia tarehe 13 hadi tarehe 23 Januari, 2020 ambapo wagonjwa waliopatiwa matibabu ni 152. Kati ya hao wagonjwa 74 walipata huduma kutoka kwa madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama na wagonjwa 78 walipata huduma kutoka kwa madaktari bingwa wa upasuaji. Aidha kati ya wagonjwa 152, wagonjwa 24 walifanyiwa upasuaji ambapo ni sawa na asilimia 96.
“Lengo kubwa la kliniki tembezi ilikuwa ni kuwajengea uwezo madaktari bingwa walioko katika hospitali ya wilaya, kuwezesha baadhi ya mashine zilizopo katika hospitali ya wilaya kuweza kuzitumia kwa usahihi zaidi kwa ajili ya upasuaji mkubwa, pia kuwasaidia wagonjwa hasa akina mama wenye matatizo ya uzazi” alisema Mganga Mfawidhi katika Hospitali ya Jakaya Mrisho Kikwete, Dr. Mohamed Mkumbwa.
Kadhalika, daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama na uzazi kutoka katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Dr. Mfaume Salum na Dr. Frank Martin Sudai ambae ni Daktari Bingwa wa Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Maweni–Kigoma, wamesema walifanikiwa kufanikisha hatua zote za upasuaji salama, na kufanikiwa kufikisha huduma za kibingwa kwa wananchi lakini pia changamoto walizokutana nazo ni pamoja na wapo baadhi ya wagonjwa waliopangiwa kurudi kwa ajili ya upasuaji lakini hawakurudi kutokana na uelewa mdogo wa masuala ya afya, uchumi, pia wengine hawakuwa vizuri kiafya kwa ajili ya upasuaji.
Pia madaktari bingwa walipendekeza kliniki tembezi kuwa endelevu ambapo ifanyike kila robo mwaka, pia watumishi wa afya waendelee kutoa elimu kwa wananchi na kuendelea kutoa hii huduma ya kibingwa katika ngazi ya wilaya.
Nao wagonjwa ambao ni wanufaika katika huduma ya kliniki tembezi wameushukuru uongozi wa Hospitali ya Jakaya Mrisho Kikwete kwa kusogeza huduma ya kibingwa katika hospitali ya wilaya ambapo huduma hii imesaidia wajonjwa wengi hasa akina mama na kutoa rai kuwa huduma hii iwe endelevu ili kupunguza gharama za kwenda hospitali ya Mkoa kwa ajili matibabu.
23/01/2020
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa