Wajumbe wa CMT Halmashauri ya wilaya ya Kishapu imetembelea na kukagua miradi ya maendeleo iliyofanyika tarehe 27/04/2020 na kuongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kishapu Sostenes mbwilo.
Katika ziara hio miradi ya maendeleo iliyokaguliwa ni pamoja na Ukamilishaji wa jengo la RCH. Hospitali ya Wilaya ya Jakaya Mrisho Kikwete lililotengewa kiasi cha shiingi 100,000,000/= ambapo jengo hilo liko kwenye hatua za mwisho za ujenzi. Wajumbe walishauri Fundi ajitahidi kumalizia ujenzi kulingana namakataba ulivyo.
Mradi mwingie uliyotembelewa ni pamoja na Ukamilishaji wa Ofisi ya Mtendeji wa Kata Mwamalasa ambapo makadirio ya Mhandisi ni kiasi cha fedha shilingi 45,000,000= lakini fadha iliyotolewa na Halmashauri ni Shilingi 15,000,000/= na nyingine ni nguvu za wananchi. Wajumbe walishauri kuwa Mhandisi aandae makadirio BOQ ambayo ni halisi ili kumalizia ujumbe huo pia walishauri vyoo vijengwe.
Aidha mradi mwingine ulitembelewa ni pamoja na Jengo la Resource Centre Mwamalasa ambapo katika uhalisia wake jingo lilionekana liko wazi halitumiki kwa matumizi yaliyokusudiwa wakati linajengwa ambapo walishauri kuwa viongozi wa kata ya Mwamalasa ilete maombi Halmashauri ya Wilaya ili jingo hilo libadilishwe matumizi liwe bweni au kituo cha Afya. Pia eneo la shamba darasa katika kijiji cha Mwandoma ambapo wajumbe walifika na kuona eneo hilo.
Pia mradi mwingine ni pamoja na Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu shule ya Msingi Imala Bupina. Mradi huu wa Nyumba ya Mwalimu ni vyumba viwili (two-in-one) na mabanda ya nyuma uliogharimu jumla ya shilingi 25,000,000/= wajumbe walipongeza ubora wa mradi huo ambapo ujenzi unaendelea.
Kadhalika, Ujenzi wa Kituo cha Afya Shagihilu ambao una jumla ya shilingi 10,000,000/= na wajumbe walishauri jengo hilo lijengwe kwa viwango sahihi ambapo Mganga Mkuu ameomba Wizara ya Fedha shilingi 50,000,000/= kumalizia ujenzi.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa