Inaundwa na vitengo viwili saidizi yaani, kitengo cha barabara na majengo. Ilianza rasmi kutoa huduma zake kwa jamii wakati wa kuanzishwa kwake tarehe 01/07/2006 wakati huo ikiwa na watumishi wake watatu waliotwaliwa kutoka Halmashauri mama ya Shinyanga vijijini.Watumishi hawa walikuwa ni Eng. P.Malimi,mkuu wa idara,Leonard N.Machiya,fundi sanifu na msaidizi pekee na Mikael N.Mpanduji,dereva (Marehemu).
Waajiriwa wengine wapya wa kwanza mwaka huo 2006 walikuwa ni Eng. Leonard B.L.Mashamba (Marehemu), aliye kuwa mkuu wa idara baada ya kuacha kazi kwa kustaafu kwenye utumishi wa umma kwa aliyekuwepo wakati huo ndugu P.Malimi na ndugu Richard Kachwele (Fundi sanifu uhandisi wa ujenzi),pamoja na ndugu Maduhu V.Fundi (Fundi sanifu uhandisi wa ujenzi) ambaye baadaye mwaka 2013 alihamia Halmashauri ya wilaya ya Meatu.
Kwa sasa idara ya ujenzi ya wilaya ya kishapu imekua na kuwa kubwa yenye watumishi wapatao wanane (08). Idara inavyo vitengo vikuu viwili tofauti , yaani kitengo cha barabara na majengo. Pamoja na vitengo hivi,idara husimamia na kuratibu pia shughuli za uendeshaji na usimamizi wa mitambo na magari yanayomilikiwa chini ya mamlaka za Serikali za mitaa ambayo ni mali ya Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.
II. TAARIFA ZA WATUMISHI NA WASIFU WAO KITAALUMA
Idara ya ujenzi ya wilaya ya Kishapu sasa ina Wahandisi na Mafundi sanifu wenye sifa na walio fuzu vyema ambao ni wachapakazi wenye bidii na nguvu ,wenye historia,uwezo majukumu na elimu mbalimbali. Idara inao wahandisi wanne (04) waliosajiriwa kwenye Mamlaka ya bodi ya Wahandisi (ERB);ambao ni Eng. Samson Pamphili (P.E), B.SC-CIVIL-UDSM( Mhandisi wa Wilaya na mkuu wa idara), Eng.Chiyando M.Matoke (G.E),B.E-CIVIL, D.I.T-DAR; (Mkuu wa kitengo cha barabara), Eng.Gemmastella Issack (G.E), B.E-CIVIL, MIST-MBEYA; (Mkuu wa kitengo cha majengo) na Eng.Richard Kachwele (G.E),B.E-CIVIL,D.I.T/STJUIT-DAR.
Sambamba na hawa wapo pia mafundi sanifu walio fuzu vyema, wenye elimu na ujuzi mzuri pamoja na uzoefu wa kitaalam. Hawa ni Leonard N.Machiya (Fundi sanifu mkuu,uhandisi wa ujenzi), CDTE-MISUNGWI, MWANZA; Victoria Pamba (Fundi sanifu uhandisi wa ujenzi), CDTE-MISUNGWI, MWANZA; Godson B. Katuba (Fundi sanifu uhandisi wa ujenzi), CDTE-MISUNGWI, MWANZA; and Paul S. Maganga (Fundi sanifu uhandisi wa mitambo na magari).A.T.C-ARUSHA.
III.0 WAJIBU NA MAJUKUMU YA UWAJIBIKAJI WA IDARA YA UJENZI NA VITENGO VYAKE
Idara ya ujenzi ya umma ya wilaya ya kishapu pamoja na vitengo vyake ina wajibika katika majukumu ikiwa na malengo ya kutoa huduma zake za jamii kwa ajili ya kuinua maendeleo ya kiuchumi wa jamii katika wilaya kama ilivyo kusudiwa katika kuanzishwa kwake
IV.0 MATARAJIO YA IDARA YA UJENZI YA WILAYA YA KISHAPU
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa