Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Josephat Limbe akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani cha kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya Kata kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026, kuanzia Oktoba hadi Disemba 2025 kikao kilichofanyika Januari 27,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imefanya kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya Kata kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026, kuanzia Oktoba hadi Disemba 2025.
Kikao hicho kimefanyika Januari 27, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, ambapo taarifa zilizowasilishwa zimegusa sekta muhimu za maendeleo na ustawi wa wananchi.
Miongoni mwa sekta zilizowasilisha taarifa ni pamoja na Afya, Barabara, Maji, Umeme, Elimu, Biashara na Viwanda, Mifugo, Utawala, Udhibiti wa Taka pamoja na Kilimo, ambapo kila sekta imeeleza mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizopo na mikakati ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma H. Mohamed akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani cha kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya Kata kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026, kuanzia Oktoba hadi Disemba 2025 kikao kilichofanyika Januari 27,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Kupitia Baraza hilo, Waheshimiwa Madiwani walipata fursa ya kujadili kwa kina utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika Kata zao, kutoa maoni, ushauri na mapendekezo yatakayosaidia kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika ngazi zote za Halmashauri.
Aidha, imeelezwa kuwa kikao cha Baraza la Madiwani kitaendelea kesho Januari 28, 2026, ambapo mijadala zaidi itaendelea pamoja na kupitishwa kwa maazimio yatakayotoa mwelekeo wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kipindi kijacho.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Enock Reuben akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani cha kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya Kata kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026, kuanzia Oktoba hadi Disemba 2025 kikao kilichofanyika Januari 27,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani cha kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya Kata kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026, kuanzia Oktoba hadi Disemba 2025 kikao kilichofanyika Januari 27,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo















Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa