• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utawala
      • Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya jamii
      • Afya
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Tehama
      • Utamaduni, Sanaa na Michezo
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Usafi wa Mazingira na Udhibiti Taka
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Kilimo na Mifugo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya picha na video za shughuli za maendeleo

CPA. MAKALA AIPONGEZA SERIKALI MAENDELEO KISHAPU – BUTONDO AOMBA DED ASIONDOLEWE

Posted on: May 23rd, 2025

Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa Taifa, Cpa.Amos Makala, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kusogeza huduma muhimu za kijamii kwa wananchi wa Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mei 23, 2025, katika Kata ya Maganzo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Cpa. Makala amesema kuwa Serikali imetekeleza kwa vitendo ahadi zake kwa wananchi wa Kishapu, hususan katika sekta ya maji.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoani Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akimkaribisha Cpa.Makala Mkoani humo kutokea Mkoai Simiyu katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama hicho Mei 23,2025 Kata ya Maganzo  Wilayani Kishapu.

“Nilipokuwa Naibu Waziri wa Maji, nilipokea kilio kikubwa kutoka kwa wananchi wa Kishapu kuhusu changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo .

Leo hii Serikali imetenga mabilioni ya fedha kutatua changamoto hiyo jambo linaloleta matumaini na maendeleo kwa wananchi,” amesema Makala.

Ameongeza kuwa Wilaya ya Kishapu imeendelea kuimarika kimaendeleo kwa kasi kubwa na kwamba wananchi wake wanaonesha bidii ya dhati katika kuchangia maendeleo yao.

“Kishapu niliyoiona miaka michache iliyopita siyo hii ya leo. Mji wa Maganzo umekua, watu wameongezeka, na shughuli za kiuchumi na biashara zimeimarika sana,” amesema.

Katika kuonesha kutambua mchango wa wananchi Cpa.Makala amewataka waendelee kuiamini Serikali na kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi mkuu ujao mwezi Oktoba  kwani ni haki yao ya kikatiba.

Cpa.Amos Makala akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Kata ya Maganzo katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mei 23,2025

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniface Butondo ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika sekta mbalimbali ndani ya kipindi cha miaka minne akisisitiza kuwa Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 3 katika elimu ambapo zaidi ya madarasa 210 yamejengwa katika shule za msingi na yote yamewekewa madawati.

“Katika Kata ya Maganzo tumefanikisha ujenzi wa kituo cha watoto wenye mahitaji maalum kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 220, na kituo hicho kinaendelea kutoa huduma kwa mafanikio makubwa,” amesema Mhe.Butondo.

Akizungumzia huduma ya maji, Mhe. Butondo amesema kuwa mwaka 2021 ni Kata 3 tu kati ya 29 zilikuwa na huduma ya maji, lakini sasa ni jumla ya Kata 21 zina huduma hiyo kupitia miradi ya Ziwa Viktoria na visima.

“Katika bajeti ijayo tumeidhinishiwa zaidi ya shilingi bilioni 16.5 kwa ajili ya kukamilisha usambazaji wa maji katika Kata za Mondo, Busangwa, Mwasubi, Bunambiyu na Sekebugolo,” ameongeza.

Kwa upande wa miundombinu amesema kuwa mtandao wa barabara umeongezeka kutoka kilomita 675 mwaka 2021 hadi kufikia kilomita 1,100 mwaka huu, huku bajeti ya barabara ikiongezeka kutoka milioni 900 hadi bilioni 2.5.

Aidha, amesema idadi ya vijiji vilivyopata umeme imeongezeka kutoka 48 hadi 117, jambo linaloonesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.

Mbunge huyo amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, kwa utendaji bora wa kazi na uongozi wa karibu na wananchi, huku akisisitiza kuwa mafanikio ya Halmashauri hiyo yanatokana pia na usimamizi mzuri wa Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Emmanuel Johnson.

“Mkurugenzi wetu Bw. Emmanuel Johnson ametufikisha mbali kwa kuboresha ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi bilioni 1.5 hadi bilioni 3.4. Tunaomba aendelee kupewa nafasi ya kuwatumikia wananchi wetu wa Wilaya  ya Kishapu kwani amekuwa chachu ya maendeleo katika Halmashauri hii" amesema Mbunge Butondo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI December 22, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 21, 2025
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • RC MHITA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI NA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KISHAPU.

    January 10, 2026
  • RC MHITA AWATAKA MADIWANI KISHAPU KUDUMISHA USHIRIKIANO NA MSHIKAMANO - NGUZO KUFANIKISHA MIPANGO YA MAENDELEO.

    December 19, 2025
  • DED JOHNSON ATOA MAELEKEZO MUHIMU KWA MADEREVA

    December 19, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WAMTEUA MWENYEKITI MPYA HALMASHAURI YA WILAYA KISHAPU

    December 03, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa