• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Nyaraka
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • Matangazo
    • Sheria ndogo ya ushuru wa huduma
    • Mifumo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
      • Uvuvi wa Samaki katika Bwawa la Songwa, Bwawa mhumbu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Mhe. William Luhende Jijimya - Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Francis Manyanda - Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Joel Ndettoson - Diwani kata ya Kishapu
      • Mhe. Mohamed Aman - Diwani kata ya Ndoleleji
      • Mhe. Lucas Nkende - Diwani kata ya Mwamashele
      • Mhe. Pontias Daud - Diwani kata ya Mwataga
      • Mhe. James Kasomi - Diwani kata ya Bubiki
      • Mhe. Bushi Mpina - Diwani kata ya Mwamalasa
      • Mhe. Nyama Kisinza - Diwani kata ya Somagedi
      • Mhe. Mashini W. Washima - Diwani kata ya Uchunga
      • Mhe. Anderson Mandia - Diwani kata ya Ukenyenge
      • Mhe. Edward Manyama - Diwani kata ya Kiloleli
      • Mhe. Reuben Siyabo - Diwani kata ya Bupigi
      • Mhe. Bujiku Nyanda - Diwani kata ya Mwaweja
      • Mhe. Michael Paul - Diwani kata ya Shagihilu
      • Mhe. Luhende S. Luhende - Diwani kata ya Lagana
      • Mhe. Richard Dominico - Diwani kata ya Talaga
      • Mhe. James Kamuga - Diwani kata ya Igaga
      • Mhe. Lameck Nsubata - Diwani kata ya Itilima
      • Mhe. Mpemba Malangahe - Diwani kata ya Bunambiyu
      • Mhe. Makenzi Charles - Diwani kata ya Busangwa
      • Mhe. Nestory Kalugula - Diwani kata ya Ngofila
      • Mhe. Lwinzi Kidiga - Diwani kata ya Maganzo
      • Mhe. Samson Gelewa - Diwani kata ya Mwasubi
      • Mhe. Sarah Marco - Diwani kata ya Idukilo
      • Mhe. Enock Bundala - Diwani kata ya Masanga
      • Mhe. Thabidha Mmbando - Diwani kata ya Mwakipoya
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri
  • miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
  • Kituo Cha Habari
    • maktaba ya picha
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa za Vyombo vya Habari
  • Maeneo
    • Kata
      • Orodha ya Kata
    • Tarafa
      • Orodha ya Tarafa
    • Vijiji
      • Orodha ya Vijiji

DC KISHAPU AFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA

Posted on: August 26th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambae pia ni mgeni rasmi wa hafla ya kilele cha mafunzo ya jeshi la akiba Mhe.Peter Masindi (kushoto) akipitishwa kukagua gwalide la wahitimu 37 na Mkufunzi na Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilayani humo Meja. Linus Elias (kulia) Agosti 26,2025 katika viwanja vya Jengoni Kata ya Ukenyenge

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi amewaasa wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba Wilayani humo kuutunza ujuzi waliopata,kudumisha amani na kutetea maslahi ya Taifa.

Mhe.Masindi ametoa wito huo Agosti 26,2025 katika hafla ya kufunga mafunzo ya jeshi la akiba yaliyofanyika katika uwanja wa Jengoni Negezi Kata ya Ukenyenge na kusema kuwa serikali ina matumaini makubwa kuwa wahitumi hao watakuwa mfano wa kuigwa katika jamii na kuwa chachu ya mabadiliko.

"Vijana wangu leo hii tunashuhudia mkihitimu mafunzo haya ya jeshi la akiba, leo ni siku yenu muhimu inayoingia katika kitabu cha historia ya maisha yenu" amesema Masindi.

"Nimeambiwa awali wakati mnaanza mafunzo haya mnamo tarehe 30,4,2025 mlikuwa 46, lakini kwa bahati mbaya wengine wakaishia njiani na sasa mnahitimu mkiwa jumla yenu 37  bila shaka hii ni faraja kubwa kwetu, sasa na nyinyi hakikisheni mnazingatia miiko na maadili mliyofundishwa na wakufunzi wenu itawasaidia kuaminika na kufanikiwa sana" ameongeza Mkuu huyo wa Wilaya

Mshauri wa jeshi la akiba Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Meja.Linus Elias

Masindi Amesisitiza kuwa serikali inatarajia kuwa wahitimu hao watakuwa mabalozi wazuri wa mafunzo hayo na kujijengea imani na heshima katika jamii huku akiwataka kuweka mbele suala la uzalendo, uadilifu na nidhamu zaidi sana wawe na uvumilivu na kuibua fursa za biashara zitakazowainua kiuchumi.

Pia ametumia jukwaa hilo kuwahakikishia wahitimu kuwa, serikali inatambua changamoto ya ajira inayowakabili na kusema kuwa tayari Uongozi wa Wilaya unafanya jitihada za kuwasiliana na vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na taasisi za serikali zenye mahitaji ya vijana wenye sifa za mafunzo ya aina hiyo ili watoe kipaumbele katika ajira pindi zitakapojitokeza.

Kwa upande wake mshauri wa Jeshi la akiba Wilayani humo Meja.Linus Elias amezipongeza jitihada za ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi  kuhakikisha mafunzo hayo yanafanyika kwa namna moja ama nyingine huku akisema wamefanikiwa kuwajengea uzalendo,nidhamu,kushiriki shughuli za kiuchumi,utu na ulinzi kulisaidia Jeshi la Kujenga Taifa JKT,Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ pindi watakapohitajika.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Bw.Emmanuel Johnson amewapongeza wahitimu hao kwa uvumilivu na kuwataka kujiunga kwenye vikundi ili wapate mkopo wa 10% na kujikwamua kiuchumi.

"Kuhusu suala la Kombati ninaahidi kugharamikia kombati zao pamoja na kuwapa kipaumbele kwenye suala la ulinzi kwenye ofisi zetu za umma" Amesema Johnson.

Gwalide la wahitimu vijana wa kiume 37 wa jeshi la akiba wakitoa kiapo kabla mafunzo hayo hayajafungwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambaye pia ni Mgeni rasmi wa hafla hiyo Mhe.Peter Masindi iliyofanyika katika viwanja vya Jengoni Kata ya Ukenyenge Wilayani humo Agosti 26,2025

Jumla ya wahitimu 37 wametunukiwa vyeti vya kozi ya mafunzo ya Jeshi la akiba yaliyoanza mwezi Aprili 30,2025 wote wakiwa wavulana.

Sambamba na hayo Mkuu wa Wilaya amefanya na kuhitimisha ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Tarafa ya Negezi katika Kijiji cha Ukeyenge,Mwaweja na Mwamadulu huku akiwataka watendaji kuhakikisha wanawatumikia wananchi ipasavyo na wananchi kuunga juhudi za maendele zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Masindi ataendelea na ziara yake katika Tarafa ya Mondo Kesho Kijiji cha Nyasamba,Mwajiningu na Itongoitale.

Matangazo

  • TAARIFA YA MTIRIRIKO WA FEDHA KWA KIPINDI KILICHOISHIA TAREHE 30 JUNE. 2022 August 14, 2023
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI November 03, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili September 20, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

    November 21, 2025
  • WATUMISHI KISHAPU WAPEWA MAFUNZO YA ELIMU YA FEDHA NA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI

    November 20, 2025
  • DC,DED NA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA KISHAPU WAUNGANA NA WANANCHI KUPIGA KURA

    October 29, 2025
  • WASIMAMIZI WA VITUO KISHAPU WAONYWA KUTOKUWA CHANZO CHA MIGOGORO

    October 27, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa