• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Nyaraka
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • Matangazo
    • Sheria ndogo ya ushuru wa huduma
    • Mifumo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
      • Uvuvi wa Samaki katika Bwawa la Songwa, Bwawa mhumbu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Mhe. William Luhende Jijimya - Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Francis Manyanda - Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Joel Ndettoson - Diwani kata ya Kishapu
      • Mhe. Mohamed Aman - Diwani kata ya Ndoleleji
      • Mhe. Lucas Nkende - Diwani kata ya Mwamashele
      • Mhe. Pontias Daud - Diwani kata ya Mwataga
      • Mhe. James Kasomi - Diwani kata ya Bubiki
      • Mhe. Bushi Mpina - Diwani kata ya Mwamalasa
      • Mhe. Nyama Kisinza - Diwani kata ya Somagedi
      • Mhe. Mashini W. Washima - Diwani kata ya Uchunga
      • Mhe. Anderson Mandia - Diwani kata ya Ukenyenge
      • Mhe. Edward Manyama - Diwani kata ya Kiloleli
      • Mhe. Reuben Siyabo - Diwani kata ya Bupigi
      • Mhe. Bujiku Nyanda - Diwani kata ya Mwaweja
      • Mhe. Michael Paul - Diwani kata ya Shagihilu
      • Mhe. Luhende S. Luhende - Diwani kata ya Lagana
      • Mhe. Richard Dominico - Diwani kata ya Talaga
      • Mhe. James Kamuga - Diwani kata ya Igaga
      • Mhe. Lameck Nsubata - Diwani kata ya Itilima
      • Mhe. Mpemba Malangahe - Diwani kata ya Bunambiyu
      • Mhe. Makenzi Charles - Diwani kata ya Busangwa
      • Mhe. Nestory Kalugula - Diwani kata ya Ngofila
      • Mhe. Lwinzi Kidiga - Diwani kata ya Maganzo
      • Mhe. Samson Gelewa - Diwani kata ya Mwasubi
      • Mhe. Sarah Marco - Diwani kata ya Idukilo
      • Mhe. Enock Bundala - Diwani kata ya Masanga
      • Mhe. Thabidha Mmbando - Diwani kata ya Mwakipoya
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri
  • miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
  • Kituo Cha Habari
    • maktaba ya picha
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa za Vyombo vya Habari
  • Maeneo
    • Kata
      • Orodha ya Kata
    • Tarafa
      • Orodha ya Tarafa
    • Vijiji
      • Orodha ya Vijiji

DC KISHAPU AKABIDHI MATREKTA 4 KWA WAKULIMA YENYE THAMANI YA MILION 238 KISHAPU ,ASISITIZA NIDHAMU YA MAREJESHO

Posted on: September 25th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi akiendesha trekta wakati akikabidhi Kwa wakulima wanne yenye thamani ya Tsh. 238,400,000 Kwa mkopo kutoka Banki ya NMB Wilayani humo Septemba 25,2025

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, amewakabidhi wakulima wanne Wilayani humo matrekta yenye thamani ya Shilingi 238,400,000/=, yaliyopatikana kupitia mkopo nafuu kutoka Benki ya NMB.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika Septemba 26, 2025, katika viwanja vya Benki ya NMB Wilayani humo Masindi amesema hatua hiyo ni chachu ya kuwaletea wamiliki wa matrekta hayo ongezeko la kiuchumi kupitia kilimo cha kisasa.

Meneja Benki ya NMB Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Alexander Macheko akizungumza wakati Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi akikabidhi Kwa wakulima wanne matrekita yenye thamani ya Tsh. 238,400,000 Kwa mkopo kutoka Banki ya NMB Wilayani humo Septemba 25,2025

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia NMB imetoa mikopo kwa riba nafuu ya asilimia 9. Tuyatumie kwa malengo ya kuongeza kipato cha familia huku mkikumbuka kurejesha mikopo hiyo kwa mujibu wa mkataba,” amesema Masindi.

Ameongeza kuwa serikali ya Awamu ya Sita inatambua thamani ya mkulima kwa kuwa sekta ya kilimo ni mhimili wa pato la taifa, na hivyo wamiliki wa matrekta wanapaswa kuwa mfano wa kuhamasisha matumizi ya teknolojia badala ya kilimo cha jembe la mkono na kutumia mifugo.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi(katikati),Meneja Mwandamizi wa Mauzo ya bidhaa za kidgitali NMB Makao makuu(kushoto) na Meneja wa Benki ya NMB Wilayani Kishapu Alexander Macheko baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuwaabidhi Wakulima Wanne matrekta ya kulimia yenye thamani ya Tsh.238,400,000 Septemba 25,2025

Aidha, amewataka wamiliki wa matrekta hayo kuwashirikisha vijana kwa kuwaelezea faida za kilimo cha kisasa kupitia zana hiyo ili nao watumie fursa hiyo kujikwamua kiuchumi.

“Vijijini mnakokaa tangazeni huduma za kulima kwa trekta. Wakulima watawafuata, ninyi mtaongeza kipato, familia zenu zitapata nafuu na marejesho ya mkopo hayatakuwa kikwazo,” amesisitiza

Kwa upande wake, Meneja wa Banki ya NMB Wilayani humo  Alexander Gabriel Macheko, amesema lengo la kutoa mikopo hiyo ni kusaidia kuinua sekta ya kilimo na kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi.

“Tunaamini wamiliki hawa wanne watahamasisha jamii zao kuhusu urahisi na faida ya kutumia trekta. NMB pia inatoa mikopo kwa wafugaji wanao nenepesha mifugo, wajasiriamali wadogo ili kuinua biashara zao na watumishi wapya ambao hawajathibitishwa kazini, ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi,” amesema Macheko.

Nao wakulima walionufaika na mkopo huo akiwemo Sagala Luminu, Magida Luahu, Saba Kwihula na Machiya Mhuli, wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutambua mchango wa wakulima, wakibainisha kuwa mikopo hiyo yenye masharti nafuu itawaondolea changamoto ya muda mwingi ambapo awali walikuwa wakitumia jembe la mikono na mifugo kama Punda na Ng'ombe na sasa itawasaidia kuongeza tija kwenye kilimo.

Matangazo

  • TAARIFA YA MTIRIRIKO WA FEDHA KWA KIPINDI KILICHOISHIA TAREHE 30 JUNE. 2022 August 14, 2023
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI November 03, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili September 20, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

    November 21, 2025
  • WATUMISHI KISHAPU WAPEWA MAFUNZO YA ELIMU YA FEDHA NA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI

    November 20, 2025
  • DC,DED NA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA KISHAPU WAUNGANA NA WANANCHI KUPIGA KURA

    October 29, 2025
  • WASIMAMIZI WA VITUO KISHAPU WAONYWA KUTOKUWA CHANZO CHA MIGOGORO

    October 27, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa