
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi amekutana na wadau wa zao la pamba katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa SHIRECU, kwa lengo la kujadili maandalizi ya ununuzi wa pamba kwa msimu mpya wa mwaka 2025/2026.

Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga David Mashauri.
Kikao hicho kimewakutanisha wawakilishi wa wakulima, wanunuzi, viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS), maafisa ugani pamoja na wataalamu kutoka taasisi mbalimbali, ambapo masuala muhimu kuhusu bei ya pamba, mizani, ubora wa zao, na changamoto za ununuzi yamejadiliwa kwa kina.

Masindi amesisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya wadau wote ili kuhakikisha kuwa mkulima ananufaika ipasavyo na juhudi zake, huku akielekeza kuhakikisha mizani zote zinazotumika ni sahihi na zimesajiliwa rasmi.
“Serikali inataka kuona wakulima wananufaika, na hakuna sababu ya mkulima kudhulumiwa kutokana na uzito usio sahihi au ucheleweshaji wa malipo,” amesisitiza Masindi.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri David Mashauri amesema serikali inayompango wa dhati kuhakikisha mkulima ananufaika na makampuni ambayo hayajaomba maeneo ya kununua pamba waje kwa wingi na serikali itawapa maeneo ya uwekezaji.
Kikao hicho ni sehemu ya jitihada za Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu katika kuimarisha sekta ya kilimo na kuhakikisha kuwa zao la pamba linaendelea kuwa chanzo kikuu cha uchumi kwa wakazi wa eneo hilo.

Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa