
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga (wa kwanza kulia) akimkabidhi kufuri kiongozi wa Amcos ya Mwasubi Gole Mashine(wa pili kutoka kulia)kufuri la ghala la Bunambiyu watakalolitumia kwa mwaka mmoja huku wakianzisha ujenzi wa ghala kwenye Kata yao Mei,16,2025
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter amefanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mwasubi, Kata ya Mwasubi wenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika huduma za kijamii.

Katika mkutano huo, uliofanyika Mei 16,2025 Mhe. Masindi amesisitiza wakazi wa Kata ya Mwasubi umuhimu wa kujenga ghala la kisasa kwa ajili ya kuhifadhi pamba ili kuongeza thamani na kuimarisha kilimo cha zao hilo muhimu katika eneo lao.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwasubi Kata ya Mwasubi Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Gesa Kija akifuatilia mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo na wananchi wa kijiji hicho wenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili mnamo Mei 16,2015.
Ameeleza kuwa uwepo wa ghala hilo utasaidia wakulima kuhifadhi pamba kwa usalama, kuepuka hasara na kuongeza kipato hivyo kwa msimu 2025/2026 Mwasubi watapewa ghala moja kutoka Bunambiyu kwa ajili ya shughuli za pamba kisha wajitegee.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwasubi Kata ya Mwasubi kwenye mkutano wa hadhara wenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto za kijamii zinazowakabili Mei 16 2015 Kijini humo.
Mhe. Masindi pia ametoa onyo kwa watu wachache wanaotishia amani na utulivu katika Kata ya Mwasubi na Bunambiyu, akisema kuwa serikali haitawavumilia watu wanaochochea migogoro au vurugu.
Katika hatua nyingine, amewahimiza wananchi kuanza ujenzi wa boma la zahanati huku akiahidi kuwa serikali itahakikisha inakamilisha ujenzi huo pindi hatua za awali zitakapokamilika.

Amesisitiza kuwa maendeleo ni jukumu la kila mwananchi na si ya serikali peke yake hivyo kwa wakulima wenye uwezo wa kifedha wanunue dawa za kuua wadudu waharibifu wa pamba badala ya kusubiri msaada wa serikali.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewakumbusha wananchi kuwa urithi wa kweli ni elimu, akisema: “Urithi wa mali mara nyingi huleta maafa, lakini elimu ni urithi wa kudumu unaomkomboa mtu.”

Amesema ushirikiano kati ya serikali na wananchi ndio njia bora ya kufanikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Mkutano huo umetoa fursa kwa wananchi kueleza changamoto zao, huku wengi wakionesha matumaini makubwa juu ya hatua zinazochukuliwa na serikali ya Wilaya ya Kishapu.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Joseph Swalala (wa kwanza kushoto) na mtalamu wa kilimo na ushirika wa Halmashauri hiyo wakifuatilia mkutano wa Mkuu wa Wilaya hiyo kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Kijiji cha Mwasubi Kata ya Mwasubi Wilayani humo.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa