Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkaoni Shinyanga Mhe.Peter Masindi ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya lishe Wilaya amewataka watendaji wa Kata kusimamia kwa makini suala la lishe kwenye maeneo yao.
Masindi ameyasema hayo Mei 8,2025 kwenye kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji wa afua za lishe ngazi ya Wilaya,Kata na Vijiji kwa kipindi cha robo ya tatu Jan-Mach 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Kata hizo ni Sekebugolo,MwaduiLohumbo,Bupigi,Bubiki,Bunambiyu,Kishapu,Mwamashele na Uchunga amewataka Watendaji hao kufanya kazi kwa mujibu wa sheria,kanuni,taratibu na miongozi wa kazi zao huku wanafunzi wa shule zote za msingi na sekondari wakipata chakula mashuleni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Emmanuel Johnson amewahimiza watendaji wote kuongeza juhudi katika kutoa elimu,kuhamasisha nakufuatilia wananchi na jamii yote kuzingatia lishe majumbani kwao na mashuleni pia.
ameongeza Wilaya ya Kishapu inajumla ya shule za msingi na sekondari 168 na hadi sasa zinazopata chakula ni 152 sawa na 90.5% hivyo amesisitiza kipindi cha robo ijayo asilimia hiyo iongezeke na kufikia 100%.









Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa