• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Nyaraka
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • Matangazo
    • Sheria ndogo ya ushuru wa huduma
    • Mifumo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
      • Uvuvi wa Samaki katika Bwawa la Songwa, Bwawa mhumbu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Mhe. William Luhende Jijimya - Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Francis Manyanda - Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Joel Ndettoson - Diwani kata ya Kishapu
      • Mhe. Mohamed Aman - Diwani kata ya Ndoleleji
      • Mhe. Lucas Nkende - Diwani kata ya Mwamashele
      • Mhe. Pontias Daud - Diwani kata ya Mwataga
      • Mhe. James Kasomi - Diwani kata ya Bubiki
      • Mhe. Bushi Mpina - Diwani kata ya Mwamalasa
      • Mhe. Nyama Kisinza - Diwani kata ya Somagedi
      • Mhe. Mashini W. Washima - Diwani kata ya Uchunga
      • Mhe. Anderson Mandia - Diwani kata ya Ukenyenge
      • Mhe. Edward Manyama - Diwani kata ya Kiloleli
      • Mhe. Reuben Siyabo - Diwani kata ya Bupigi
      • Mhe. Bujiku Nyanda - Diwani kata ya Mwaweja
      • Mhe. Michael Paul - Diwani kata ya Shagihilu
      • Mhe. Luhende S. Luhende - Diwani kata ya Lagana
      • Mhe. Richard Dominico - Diwani kata ya Talaga
      • Mhe. James Kamuga - Diwani kata ya Igaga
      • Mhe. Lameck Nsubata - Diwani kata ya Itilima
      • Mhe. Mpemba Malangahe - Diwani kata ya Bunambiyu
      • Mhe. Makenzi Charles - Diwani kata ya Busangwa
      • Mhe. Nestory Kalugula - Diwani kata ya Ngofila
      • Mhe. Lwinzi Kidiga - Diwani kata ya Maganzo
      • Mhe. Samson Gelewa - Diwani kata ya Mwasubi
      • Mhe. Sarah Marco - Diwani kata ya Idukilo
      • Mhe. Enock Bundala - Diwani kata ya Masanga
      • Mhe. Thabidha Mmbando - Diwani kata ya Mwakipoya
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri
  • miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
  • Kituo Cha Habari
    • maktaba ya picha
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa za Vyombo vya Habari
  • Maeneo
    • Kata
      • Orodha ya Kata
    • Tarafa
      • Orodha ya Tarafa
    • Vijiji
      • Orodha ya Vijiji

DC MASINDI AONYA UCHAFUZI WA MAZINGIRA KISHAPU HATUA KALI KUCHUKULIWA DHIDI YAO

Posted on: September 20th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga na mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya Usafishaji Duniani ngazi ya Wilaya Mhe.Peter N. Masindi  akizungumza na Wananchi wa Wilaya hiyo baada ya zoezi la ufanyaji usafi maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za kijamii Septemba 20,2025

Wakati Dunia ikiadhimisha Siku ya Usafishaji Mazingira, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, ametoa onyo kali kwa wote wasiothamini usafi na wanaoharibu mazingira, akisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Akizungumza Septemba 20, 2025, kwenye maadhimisho ya siku hiyo ngazi ya Wilaya akiwa ndiye Mgeni rasmi, Mhe. Masindi amesema wananchi wote wana wajibu wa kutunza mazingira yanayowazunguka hususani yale yanayotoa huduma za jamii ikiwemo vituo vya mabasi, hospitali, masoko, magulio, mitaro na pembezeni mwa barabara.

Katibu Tawala Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Bi.Fatma H.Mohamed akizungumza kwenye   Maadhimisho ya siku ya Usafishaji Duniani ngazi ya Wilaya baada ya zoezi la ufanyaji usafi maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za kijamii Septemba 20,2025 huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter N. Masindi  akiwa ndiye mgeni rasmi

“Ni marufuku kuchoma moto taka kwenye mazingira ya makazi. Hakikisheni mnatunza taka na kuzipeleka dampo la muda la Shireku. Taka zinazooza mnaweza kuzichimbia kwenye mashimo kisha kutumia mboji yake kuongeza rutuba mashambani,” amesema DC Masindi.

Amesema suala la usafi ni la lazima na sio ombi, na kumuelekeza Afisa Mazingira wa Wilaya kuhakikisha vifaa vya kuhifadhia taka vinaongezwa maeneo ya barabarani, vituo vya mabasi na kuimarisha elimu ya uhifadhi wa mazingira.

Afisa Mazingira Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Cassim Saim Said akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya Usafishaji Duniani ngazi ya Wilaya baada ya zoezi la ufanyaji usafi maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za kijamii Septemba 20,2025 huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter N. Masindi  akiwa ndiye mgeni rasmi

“Asiwepo wa kuufanya mji wetu wa Kishapu kuwa mchafu. Mifuko ya plastiki ni marufuku. Ni kosa pia kutupa chupa au vifungashio vya vinywaji mitaani na mitaroni. Atakayebainika, sheria itachukua mkondo wake,” ameongeza.

Katika hatua nyingine, Mhe. Masindi amewataka wananchi kuendelea kujenga vyoo bora na vya kisasa ili kulinda afya na kupunguza uchafuzi wa mazingira, hasa kwenye vyanzo vya maji.

" Ninyi mnaosubiria watu wamelala mnaenda kutupa taka maeneo yasiyorasmi nawatumia salam serikali Iko kazini na ninyi wenye tabia ya kujisaidia na Kuhifadhia kinyesi kwenye mifuko kisha kuitupa kwenye vyanzo vya Maji ukibainika Sheria haitakuvumilia uchafu umepelekea watu wengi tuliowapenda na kutamani tuwe nao Leo hawapo Tena kwani magonjwa yasababishwayo na uchafu ikiwemo Kipindupindu yaliwaondolea uhai hivyo hatutaruhusu tena uzembe kwenye uhai wa watu" ameongeza Mkuu huyo Wilaya

Katika hatua nyingine Masindi ametoa wito kwa wananchi kila kaya kupanda miti ifikapo msimu wa mvua mwezi Novemba, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. 

Vilevile, amehimiza wananchi kushiriki kikamilifu uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 kwa amani, kwa kuchagua viongozi wenye maono ya kutatua kero za wananchi.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu, Bi. Fatma H. Mohamed, amewapongeza wananchi waliojitokeza kushiriki zoezi la usafi, akisema wameonesha mshikamano wa dhati kwa serikali.

Afisa Mazingira wa Wilaya hiyo, Cassim Salim Said, amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa usafi na kuonesha kwamba taka zina thamani endapo zitachakatwa kwa njia sahihi.

“Sasa hivi tuko kwenye dunia yenye teknolojia; kila taka inafaida. Tunahakikisha wananchi wanapata elimu ya usafi na thamani ya taka, hata wanafunzi mashuleni,” amesema Said.

Baadhi ya wakazi wa Mhunze, Josephina Methew na Cesilia Jackson, wameeleza kuwa maadhimisho hayo yamekuwa kumbusho muhimu kwa jamii kuhusu wajibu wa kutunza mazingira, kwani afya bora inategemea mazingira safi.

Ikumbukwe kuwa Septemba 10, 2025, TFS Kishapu kupitia Mhifadhi Misitu wa Wilaya, Tumaini Masatu Mwijarubi, ilitangaza mpango wa kuotesha miche 200,000 ya matunda, mbao na kivuli kwa wananchi bure ili kupambana na mabadiliko ya tabianchi kuelekea msimu wa mvua hapo baadae.

Usafi wa pamoja umefanyika maeneo mbalimbali ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mhunze, ukihusisha pia wadau wa Shirika la TCRS. Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo: “Tunza Mazingira kwa Kuzipa Taka Thamani.”

Matangazo

  • TAARIFA YA MTIRIRIKO WA FEDHA KWA KIPINDI KILICHOISHIA TAREHE 30 JUNE. 2022 August 14, 2023
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI November 03, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili September 20, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

    November 21, 2025
  • WATUMISHI KISHAPU WAPEWA MAFUNZO YA ELIMU YA FEDHA NA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI

    November 20, 2025
  • DC,DED NA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA KISHAPU WAUNGANA NA WANANCHI KUPIGA KURA

    October 29, 2025
  • WASIMAMIZI WA VITUO KISHAPU WAONYWA KUTOKUWA CHANZO CHA MIGOGORO

    October 27, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa